BAYPORT YATANGAZA WASHINDI WALIOJIPATIA UDHAMINI WA KUSOMESHWA VYUO VIKUU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BAYPORT YATANGAZA WASHINDI WALIOJIPATIA UDHAMINI WA KUSOMESHWA VYUO VIKUU

Baadhi ya washindi wa 2,000,000 katika mradi wa kuhudumia jamii wa 'Bayport Change a life’,Hassan Rajab (pili kushoto) na Rodness Milton (pili kulia) wakiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Bayport Financial Services,Dr. Ken Kwayu (kulia) pamoja na Meneja Masoko wa Bayport Financial Services,Ngula Cheyo.

Bayport Financial Services huwa kila mwaka inatoa udhamini chini ya mradi wake wa kuhudumia jamii unaotambulika kama 'Bayport Change a life’, kampuni imeamua kutoa msaada huo kwa jamii hapa nchini wa zaidi ya shilingi milioni hamsini kwa ajili ya kusaidia huduma za jamii kama vile waathirika wa majanga mbali mbali, watoto yatima, mipango ya vijiji kama vile uchimbaji wa visima vya maji safi na salama, pia kiasi cha shilingi milioni ishirini kutumika katika ukarabati wa shule za msingi kama vile Shule ya Msingi Airport mkoani Kigoma, na kuimarisha jamii kielimu kwa kutoa udhamini kwa wanafunzi wa Vyuo vikuu.

Meneja masoko na uhusiano wa kampuni hiyo Bw. Ngula Cheyo alisema kwamba, mchakato wa kuwatafuta wanafunzi wawili ambao wangeweza kunufaika na msaada wa udhamini wa mfuko wa hisani wa elimu ya juu “Bayport University Scholarship” ulianza mnamo mwezi julai, 2010, ambapo zoezi hili lilitangazwa nchi nzima na kupatikana kwa watahiniwa sitini na mbili (62) waliokuwa na vigezo takwa, kati ya hao watahiniwa, 34 walikuwa ni wa kiume na 28 walikuwa wa kike toka katika mikoa ya Tanzania bara.

Licha ya matokeo ya kidato cha sita, watahiniwa walioshiriki walitakiwa kuandika insha fupi kuelezea malengo na uelewa wao juu ya taasisi za mikopo na ni nani maishani anaemhamasisha. Bwana Ngula alisema kwamba kamati ya Bayport University Scholarship ambae mwenyekiti wake ni Dk. Ken Kwaku (Bayport Chairman) iliwachagua washindi wawili ambao ni Hassan Rajab na Rodness Milton kuwa ndio walioshinda.

Pia aliongeza kwa kusema, Bayport hutoa fursa kwa njia ya mikopo au kielimu kwa watu mbalimbali, kuwawezesha kujenga uwezo wao wa kujiendeleza na kubadilisha mwelekeo wa maisha yao. Wanafunzi hawa wameonyesha nia na mtazamo sahihi wa kujikwamua kimaendeleo kwa kupitia elimu bora ndio maana Bayport ikaamua kutimiza malengo yao.

Rodness kutoka Muleba, Bukoba anatimiza nia yake ya kua wa kipekee kwa kwenda Chuo kikuu cha Dar es salaam kuchukua masomo ya uhandisi (Chemical engineering) na kusema ya kwamba mtu anayemhamasisha ni Professor Anna Tibaijuka.

Naye Hassan kutoka Mbagala, Dar es salaam ni mwanafunzi aliyepata wastani daraja la kwanza au triple “A” katika masomo ya uchumi, Hisabati na Jografia atakayekwenda kuchukua mchepuo wa utunzaji wa fedha yaani “Bachelor in Account and finance” katika Chuo kikuu cha Mzumbe, Morogoro. Kijana huyu ana ufahamu mkubwa juu ya Taasisi za Mikopo, pia mtu anayemhamasisha ni Mwalimu wake wa Secondary, Mr. Manyilizu.

Udhamini wa wanafunzi wa vyuo vikuu uliotolewa na Bayport ni wa kiasi cha shilingi milioni mbili, Tshs. 2,000,000/= kwa kila mwanafunzi kwa kila mwaka, ambazo zitatumika katika kulipia ada za masomo (Tuition fee), malazi, lap top, manunuzi ya vifaa vitakavyotumika kielimu na matumizi mengine yatakikanayo chuoni.

Bayport Financial Services ni kampuni lililoenea katika nchi za kiafrika ambayo hutoa mikopo yenye manufaa kwa kuweza kukidhi mahitaji ya wateja wake, hasa kwa watumishi wa umma na wafanyakazi walioajiriwa katika sekta binafsi zilizo idhinishwa.

Bayport financial services inaendesha huduma zake katika nchi zifuatazo; Ghana, Zambia, Uganda, Tanzania, Afrika ya kusini na Botswana ambapo imetoa mikopo kwa wateja wapatao 300,000 kupitia matawi yake 235 na ikiwa na wafanyakazi zaidi ya 2500.

Bayport Tanzania inatoa mikopo isiyo na amana wala dhamana kwa watumishi wa umma na makampuni binafsi kupitia yaliyoidhinishwa kupitia matawi yake 43 yaliyo katika hali ya kisasa hapa nchini. Tunatazamia kukua zaidi kwa kufungua matawi mengi zaidi katika kila wilaya hapa nchini ili kuwarahisishia wateja wetu uchukuaji wa mikopo ya kukuza mitaji yao katika njia salama na za uhakika alisema Bw Ngula Cheyo.
Habari Kwa Hisani Ya Michuzi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages