UPENDO WA MAMA HADI KWA WANYAMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

UPENDO WA MAMA HADI KWA WANYAMA

Kiboko akimsukuma taratibu pundamilia mdogo hadi ng'ambo ya mto nchini Kenya.

WAGENI waliokuwa Safari Camp, sehemu ambayo filamu ya "Out of Africa" ilipigwa, walikuwa wanashangaa wakati wakishuhudia kundi kubwa la kongoni wakihama kwenda kutafuta malisho. Wakati wakiwa wanashangalia maelfu ya wanyama hao wakivuka Mto Mara, walishangaa kumwona kiboko wa kike akimwokoa mmoja wa wanyama hao ambaye alikuwa kachukuliwa na mkondo wa mto huo. Ndama mmoja wa kongoni alikuwa anapelekwa na maji hayo huku mama yake akiwa hana la kufanya. "Kwa mshangao wa kila mtu aliyekuwepo, kiboko alimwendea ndama huyo na kumsukumizia taratibu pembeni mwa mto," alisema Abdul Karim, kiongozi mkuu wa watalii katika Kituo cha Olonana, huko Masai Mara, Kenya. Ndama huyo alitweta kwa muda na kusimama kisha kukimbilia kwa mama yake.

Kiboko huyo akimwokoa kongoni.(Nyumbu)

Kazi ya kiboko huyo haikuishia hapo. Dakika kumi baadaye alimwona pundamilia mdogo akivuka eneo hilohilo la maji, akamwendea na kumsukuma taratibu ili asizame. "Lilikuwa tukio lisilosahaulika," alisema Karimu na kuongeza: "Upendo wa mama umeenea hadi kwa wanyama. "Makundi makubwa ya wanyama husafiri kati ya Kenya na Mbuga ya Taifa ya Serengeti ya Tanzania kila mwaka wakitafuta malisho mapya.

Habari Kwa Hisani Ya Global Publisher Tanzania

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages