MISS EARTH TZ AENDA VIETNAM LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MISS EARTH TZ AENDA VIETNAM LEO

KILA LA KHERI MISS EARTH WETU MZURI
Miss Earth Tanzania, Rose Shayo

MWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Miss Earth 2010, Rose Shayo
aliondoka nchini leo kwenda Vietnam huku akiwa na matumaini makubwa ya kufanya vyema katika mashindano hayo.


Akizungumza kabla ya kuondoka, Rose alisema kuwa amejiandaa vilivyo chini ya muandaaji Wake, Maria Sarungi wa Compass Communications na bila shaka atafanya vyema katika mashindano hayo.

Rose amesema kuwa haendi kuwa msindikizaji katika mashindano hayo na atafanya kila aliwezalo ili kufanya vyema kama ilivyokuwa kwa Miriam Odemba mwaka 2008 nchini Philippines.

“Najua kuna kushinda na kushindwa, mimi sitarajii kushindwa kutokana na
maandalizi yangu, nawaomba Watanzania wanipe sapoti kubwa wakati wote nikiwa kambini na siku ya mashindano,” alisema Rose.


Maria alisema kuwa, alisema mrembo huyo amejiandaa vizuri kwakuwa mashindano ya kumsaka mrembo huyo yalifanyika mapema mwaka huu.

“Mashindano ya kumsaka mrembo huyu yalifanyika tangu mwezi wa nne mwaka huu kutokana na hali hiyo alipata muda mwingi wakujiaandaa hali inayomuweka katika nafasi nzuri ya kushinda, tutarajie ushindi kwakweli,” alisema Maria.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages