ANNA MAKINDA APITISHWA NA CCM KUWANIA USPIKA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

ANNA MAKINDA APITISHWA NA CCM KUWANIA USPIKA

JUST IN:Chama cha Mapinduzi CCM Kimempitisha Anna Makinda Kuwania Nafasi ya Uspika
Bi. Anna Makinda(Pichani)amechaguliwa na Wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi kwa kura 211 kwa ajili ya kuwania Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Katika bunge lililopita Bi Anna Makinda alikua Naibu Spika ambapo Mheshimiwa Samwel Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki alikua Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waliobwagwa katika kinyang'anyiro hicho cha akina mama watatu walioteuliwa na Kamati Kuu ya CCM hapo jana kuwania kiti hicho ni bi Kate kamba aliyepata kura 15 bi Anna Abdalah aliyepata kura 14.kwa maani hiyo basi MheshimiwaAnna Makinda(CCM)kupambana na Mabere Marando(CHADEMA).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages