AMOSI MAKALLA AANZA KAZI JIMBONI KWAKE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

AMOSI MAKALLA AANZA KAZI JIMBONI KWAKE

Hili ni moja ya daraja la waenda kwa miguu ambalo lilipata msukosuko kutokana na maji yaliyosababishwa na mafuriko katika kata tano za tarafa ya Mgeta wilayani Mvomero,mbele yake ni mwenyekiti wa wilaya hiyo Kololeti Mgema.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero Amos Makalla katikati (mwenye suti Nyeusi),akimsikiliza mmoja wa wananchi wa kata ya bunduki tarafa ya mgeta wilayani Mvomero mkoani morogoro,ambaye alikuwa akielezea jinsi mafuriko yalivyoathiri moja ya daraja .ukiangalia juu unaona ni daraja .
Amos Makalla akitazama baadhi ya miundo mbinu iliyoharibiwa na mafuriko hayo
Hali halisi ndio kama mnavyoiona kuna watu wana tabu kweli kweli
AMOS MAKALLA AMBAYE NI MBUNGE WA KWANZA HAPA NCHINI KUANZA KUFANYA KAZI YAKE UBUNGE SIKU YA NOVEMBA 19 IKIWA NI SIKU MOJA MARA BAADA YA KUARISHWA KWA BUNGE MJINI DODOMA.
AMBAPO ALIFANYA ZIARA YA KTK TARAFA YA MGETA NA KUWAPA POLE WALIOPATWA NA MAFURIKO WANANCHI WA KATA TANO,MAKALLA ALITOA MILIONI 2 ZA HARAKA KUSAIDIA WANANCHI HAO WAKATI WAKISUBIRI MSAADA KUTOKA OFISI YA WAZIRI MKUU KITENGO CHA MAAFA,
Habari na PICHA ASHTON BALAIGWA,MOROGORO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages