NEO la kupumzikia wasafiri kwenye Kituo cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo Buses Terminal( UBS) linadaiwa kugeuzwa jengo la kuishi watu wasio na makazi jijini Dar es Salaam.
Ilielezwa kwamba eneo hilo kwa usiku linatumika kama makazi ya watu wasio na maeneo ya kuishi huku wengine wakibarikiwa kupata watoto kwa maisha hayo.
Akizungumza na Mwananchi jana mfanyabiashara ndani ya kituo hicho, aliyejitambulisha kwa jina la Juma Hashim, alisema eneo limebadilika kuwa eneo makazi ya watu wanaoishi.
“Ninashangaa kuona eneo kama hili limetengwa kwa ajili ya wasafiri, lakini watu hufanya makazi hasa wanaotoka mikoani na kufika halafu hawana ndugu na kungeuza humu ndani kuwa makazi yao”alisema Hashim.
Alisema eneo hilo pia limekuwa ni eneo la kuhifadhi vibaka na kuwafanya abiria wanaosubiri kuunganisha magari kesho yake , kushidwa kukaa kwa amani kwa kuhofia usalama wa mali zao.
Mwananchi ilipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa watu waliofanya makazi eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Asha Bashiri kutoka Kigoma.
Akifafanua juu ya maisha yake, Asha alisema alifika hapo akiwa na mtoto mmoja kutoka Kigoma kumtafuta mumewe miaka mitatu iliyopita, lakini mpaka sasa hajampata.
Alisema kwa ujumla wapo watu zaidi ya 30 wanaoishi na kuolewa kwenye ukumbi huo na wengine kupata watoto kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.
“Mimi nimetokea mkoani Kigoma nimekuja na mtoto wangu Karimu ili kuja kumtafuta baba yake, lakini sijafanikiwa kumpata na sina nauli ya kurudi nyumbani na mpaka sasa nimepata mtoto mwingine ambaye ni Fatuma” alisema Asha.
Hata hivyo, mwanamke huyo alikiri kwamba mazingira ya eneo hilo ni magumu kwani wanasumbuliwa na mgambo wa Jiji wanaowafukuza eneo hilo.
“Mazingira ya hapa ni magumu sana kwani wanamgambo wa jiji wanatusumbua kwa kutaka tuondoke eneo hili wakati hatuna pakwenda na wala hatuna ndugu katika mijini huu”alisema mama huyo.
Polisi wa waliopo ndani ya kituo hicho walipoulizwa walisema hawana taarifa juu ya kuwepo kwa watu wanaoishi humu.
Meneja wa UBS hakuweza kupatikana kwa jana ilki azungumzie suala hilo.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)