Taifa Stars yapigwa 1-0 na Morocco - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Taifa Stars yapigwa 1-0 na Morocco


JK akipungia mashabiki baada ya kukagua timu za Tanzania na Morocco neshno jijini Dar. Morocco walishinda 1-0 Kikosi cha Taifa Stars kilichocheza na Morocco
Waamuzi wakiingia uwanjani Wachezaji wa Morocco wakati wa nyimbo za taifa.
Hapa ni wakati wa mapumziko kwani nyimbo hizo hazikuwa
tayari kabla ya kuanza kwa mchezo. Ilikuwa bonge la noma na TFF inabidi wapigwe memo kwa kufanya madudu haya mbele ya Rais
Nahodha wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa (shoto) akisalimiana na mwenzake wa Morocco, Kharja Houssine kabla ya gemu kuanzaHekaheka langoni pa Morocco Beki wa Stars, Stephano Mwasika (kulia) akiwatoka wachezaji wa Morocco, Basser Michael na Berrabeh Mohamed. Mshambuliaji wa Morocco, Chamakh Marouane ambaye anaichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza akiipangua ngome ya Stars wakati wa mchezo wa kufuzu Fainali za Afrika uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Stars, Danny Mrwanda anayechezea soka la kulipwa huko Vietnam (katikati) akiwa amebanwa na wachezaji wa timu ya Morocco, Kharja Houssine (kulia) na Soulaimani Rachid. Picha zote na Francis Dande wa Globu ya Jamii


Timu ya Taifa ya Morocco imeweza kujipatia pointi muhimu na goli la ugenini baada ya kuifunga Taifa Stars bao 1-0 katika mchezo wao uliopita katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Alikuwa mshambuliaji Mounir El-Hamdaou wa Morocco aliyefunga bao hilo pekee la mchezo kwa shuti kali toka mguu wa kushoto, lililomshinda mlinda mlango Juma Kaseja, dakika mbili tu kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza.

Hii ilikuwa ni mwendelezo wa ratiba ya mechi za kufuzu kucheza fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika ambapo katika mechi iliyotangulia iliyochezwa nchini Algeria hapo Septemba 3, 2010, Tanzania walipata pointi muhimu ya ugenini japo walitoka sare ya bao 1 - 1 dhidi ya wenyeji wao.
Tanzania imepangwa kundi moja la D, na timu za Algeria, Morocco na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mgeni rasmi katika mechi hiyo alikuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mdau mkubwa wa michezo, Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alisitisha kampeni za uchaguzi mkuu ili kuhudhuria mechi hiyo.

credit source:
http://www.wavuti.com

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages