Leon Bahati, Songea
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete jana alisita kutoa jibu la mara moja baada ya wakazi wa wilaya mpya ya Nyasa kumbana wakitaka awaruhusu kujitenga kibiashara na maeneo mengine ya Tanzania na badala yake washirikiane na nchi jirani ya Malawi.
Kikwete alikumbana na hoja hiyo ya aina yake wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Mbambabay, eneo ambalo linakusudiwa kuwa makao makuu ya wilaya hiyo mpya.
Wakazi hao wa mji huo ulio mpakani na Malawi walisema kufanya biashara na maeneo mengine nchini kumewasababishia maisha magumu na hata kuwarudisha nyuma kiuchumi.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Nyasa, John Komba, ambaye pia ni kada wa muda mrefu wa chama hicho, ndiye aliyewasilisha hoja hiyo mbele ya Kikwete akieleza kuwa kufanya biashara na maeneo mengine ya Tanzania kumesababisha vitu kuuzwa kwa bei kubwa.
“Mfano sukari inayopatikana kimagendo kutoka Malawi inauzwa Sh 1,500 kwa kilo wakati ile inayozalishwa hapa nchini huuzwa kwa zaidi ya Sh3,000 kwa kilo,” alisema Komba, ambaye pia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM.
Habari zinasema kuwa kabla ya serikali kuzuia biashara na Malawi, sukari kutoka nchi hiyo iliyo kusini mwa Tanzania ilikuwa ikiuzwa Sh600 kwa kilo katika kipindi ambacho sukarti ya kutoka ndani ilikuwa ikiuzwa Sh2,500 kwa kilo.
Mkazi mmoja aliyeongea na Mwananchi, Erasmus Kato alisema uamuzi wa serikali kuzuia biashara na ndugu zao wa Malawi kumefanya maisha yao kuwa magumu na kuthibitisha kuwa sukari imepanda sana baada ya uamuzi huo.
Kato alisema iwapo serikali itawaruhusu kufanya biashara na jirani zao ni rahisi hata mafuta ya petroli kuuzwa Sh1,200 tofauti na bei ya sasa ya Sh1,700 kwa lita ya mafuta yanayopatikana nchini.
Lakini akijibu hoja hizo, Kikwete aliwaambia maelfu ya watu waliofurika kumsikiliza kwamba wavute subira ili serikali ikae chini na kufanyia kazi ombi lao.
Vile vile alisema kwamba serikali itawasiliana na wenzao wa Malawi kuona ni namna gani wanaweza kushirikiana katika shughuli za kimaendeleo.
Katika hatua nyingine, Kikwete aliendelea kutoa ahadi na safari hii aliwaahidi wakazi wa wilaya hiyo mpya kuwa atawapatia meli yenye uwezo wa kubeba tani 400.
Ahadi kama hiyo alishaitoa kwa wakazi wanaoishi kando ya Ziwa Victoria na Tanganyika huku akiwaponda wapinzani kwa kukejeli mpango huo.
Kikwete pia aliahidi kutatua tatizo la upungufu wa walimu katika kipindi cha miaka mitatu ijayo na kwamba kila mwaka wamepanga kupeleka walimu wapya watano katika kila shule za msingi na sekondari za kata.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)