Chadema kujenga soko ndani ya miezi mitatu - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Chadema kujenga soko ndani ya miezi mitatu


Pamela Chilongola
MGOMBEA udiwani wa Kata ya Ukonga kwa tiketi  ya Chadema, Richard Nyambacha amesema endapo atachaguliwa kuwa diwani atajenga soko la kudumu kwenye kata hiyo, ndani ya miezi mitatu.
Akizungumza juzi wakati  akihutubia mkutano uliofanyika kwenye kituo cha mabasi cha  Mombasa, Nyambacha alisema endapo wakimpa ridhaa ya kuongoza atahakikisha soko la kata hiyo, linajengwa muda wa miezi mitatu ili kuondoa kero ya muda mrefu.
Alisema atatumia maeneo ya wazi kujenga soko ili kupunguza safari za wakazi wa eneo hilo kwenda kutafuta bidhaa katika Soko la Buguruni.
“Eneo tunalo viwanja vya wazi vipo nitahakikisha ndani ya miezi mitatu tutajenga soko hata kwa kuchangishana ili tujenge soko kwenye Kata ya Ukonga ili tuondokane na usumbufu tunaoupata  kwenda kutafuta bidhaa kwenye soko la buguruni,”alisema Nyambacha.
Alisema kuhusu elimu, atashirikiana na wananchi wa kata hiyo kujua kiini cha tatizo la elimu na kupeleka katika vikao vya madiwani wa Halmashauri ya wilaya.
 “Kwa pamoja mbinu mbalimbali zitapatikana za kutafuta  fedha kwa ajili ya kutatua matatizo kama vile ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, vitabu na madawati,” alisema.
Naye Katibu Mwenezi wa Jimbo la Ukonga, Ernest Njooka alisema wanachama 56  kutoka CCM  na wawili wa TLP wamejiunga na Chadema.
Njooka alisema watahakikisha wanavunja ngome za CCM ili wapate  wanachma wengi ili kuhakikisha jimbo hilo linachukuliwa na Chadema.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages