Watuhimiwa wawili wa Uwizi,Mmoja akiwa na Kitambulisho cha Idara ya Usalama wa Taifa wadakwa Usiku Huu Kawe,Jijini Dar - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

demo-image

Watuhimiwa wawili wa Uwizi,Mmoja akiwa na Kitambulisho cha Idara ya Usalama wa Taifa wadakwa Usiku Huu Kawe,Jijini Dar

IMG_6177
Mtuhumiwa wa Uwizi aliejitambulisha kwa jina la Juma Hamis huku akiwa na Kitambulisho cha Kazi cha Idara ya Usalama wa Taifa chenye jina la Kenedy Magige,akiwa amewekwa chini ya Ulinzi mara baada ya kunaswa Usiku huu kwenye Hoteli ya Picolo,Kawe jijini Dar es Salaam,
IMG_6209
 Watuhumiwa hao wakiwa chini ya Ulinzi wa Polisi.
IMG_6215
 Mtuhumiwa wa Uwizi aliejitambulisha kwa jina la Juma Hamis huku akiwa na Kitambulisho cha Kazi cha Idara ya Usalama wa Taifa chenye jina la Kenedy Magige.
IMG_6217
 Mtuhumiwa mwenza wa Tukio hilo la Wizi,aliejitambulisha kwa jina la Takula Manyenga mwenye umri wa Miaka 28,akidhibitiwa kwa kufungwa kamba mara baada ya kukamatwa Usiku huu kwenye Hoteli ya Picolo,Kawe jijini Dar es Salaam.
IMG_6223
IMG_6224
 Watuhumiwa wote wawili wakipakiwa ndani ya Gari la Polisi kutoka katika Kituo cha Kawe,Jijini Dar es Salaam.
IMG_6228
 Watuhumiwa hao wakiwa ndani ya gari la Polisi.
IMG_6231
 Askari Polisi wakiwa eneo la tukuo kuhakikisha Usalama unapatikana eneo hilo.
IMG_6235
 Mara wakashushwa kwa muda na kuelekea kwenye Gari lao walilokuja nalo watuhumiwa hao.
IMG_6240
 Askari Polisi wakiwa na Watuhumiwa hao wakati wakiendelea na Ukaguzi ndani ya Gari hilo aina ya Toyota Prado lenye nambari za Usajili T 445 BCY.
IMG_6243
 Askari Polisi wakiendelea na Ukaguzi ndani ya Gari hilo,ambapo ndani ya Gari hilo kulikutwa na Simu zaidi ya kumi ambazo zilichukuliwa na Polisi hao.
IMG_6245
 Gari walilokuwa wakilitumia Watuhumiwa hao.
IMG_6246
 Wakipelekwa kwenye Gari la Polisi tayari kwa safari ya kwenda Kituoni.
IMG_6250
 Ulinzi mkali kwa watuhumiwa hao.
IMG_6254
Msafara wa kuelekea kituoni.
Watu wawili wanaotuhumiwa kuwa ni wezi a.k.a Wapigaji/Matapeli wamekamatwa Usiku huu kwenye hoteli ya Picolo,Kawe jijini Dar es Salaam.

Watu hao ambao wamekamatwa ni Bw. Takula Mayenga mkazi wa Mbezi Temboni na Bw. Juma Hamis ambaye ni mkazi wa Tabata wakiwa na nyaraka tofauti ikiwemo kitambulisho cha Idara ya Usalama wa Taifa, kadi za benki pamoja na simu zaidi ya kumi,wakiwa katika harakati za kumtapeli mwanadada mmoja aliejitambulisha kwa jina la Rebecca ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo cha Biashara cha CBE,Mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaa  .

Akisimulia tukio dada huyo ambaye alipatwa na tukio hilo la kutapeliwa Ijumaa ya wiki iliyopita alisema kuwa, ilikuwa ni Ijumaa iliyopita wakiwa wamekaa katika fukwe wakipunga upepo ndipo alipokuja tapeli huyo na kukaa nao na baadae walimwekea madawa ya kulevya na kuondoka na dada huyo kwenda kumtupa baharini
HABARI KWA HISANI YA MICHUZI BLOG

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Pages