LIYUMBA AKWAA BALAA JIPYA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

LIYUMBA AKWAA BALAA JIPYA



Hamida Hassan na Gladness Mallya
MNAMKUMBUKA aliyekuwa kigogo wa Benki Kuu ya Tanzania aliyefungwa jela miaka miwili kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na ufujaji wa mali za umma, Amatus Joackim Liyumba? Basi amekwaa balaa jipya, Uwazi linajua kila kitu.............
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI»

 
Amatus Joackim Liyumba.
Liyumba na mwanamke aliyedai ni mke wake, Aurelia Paulo Ngowi wamefikishana Mahakama ya Kinondoni, Dar kisa kikidaiwa ni mzee huyo kumtaka mwanamke huyo kuondoka haraka kwenye nyumba anayoishi na watoto wao wawili. Nyumba hiyo ipo Mbezi ya Afrikana, jijini Dar. Mbali na kuwa makazi, lakini sehemu ya mbele ya nyumba hiyo ni Hoteli Amjen yenye kupata wateja kila siku.
Nyumba yenyewe ndiyo hii.
Jina la Amjen linadaiwa ni muuganiko wa majina ya Amatus na Jennifer ambaye ni mtoto mmoja kati ya hao wawili wa mzee huyo.  Aurelia ndiye aliyekimbilia mahakamani kuomba msaada ambapo shauri lake lilifunguliwa kwa namba 59, 2013 mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo aliyejulikana kwa jina moja la Rugemalira. Baada ya ombi hilo, mahakama ilimwamuru Liyumba kumwacha mkewe na watoto hao waendelee kuishi kwenye nyumba hiyo mpaka shauri hilo litakapotatuliwa kisheria.
Mwanamke aliyedai ni mke wa Liyumba, Aurelia Paulo Ngowi akiwa na watoto wake.
Haikujulikana mara moja kama Liyumba anataka mkewe na watoto waondoke kwenye nyumba hiyo na yeye kwa sasa anaishi wapi.  Jitihada za kumtafuta zilifanyika, simu yake ya mkononi haikuwa hewani huku ikidaiwa kwamba namba husika haitumii tena. Baadhi ya watu wake wa karibu waliliambia Uwazi kwamba, kwa sasa Liyumba anaishi Kinondoni, Dar es Salaam lakini kupatikana kwenye simu ni ishu nyingine.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS BLOG

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages