Mheshimiwa Balozi Hamisi Kagasheki (MB)Waziri wa Maliasili na Utalii akisalimiana na wageni toka Lichinga Msumbiji.
Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) Akivalishwa Vazi la kijadi.
Baadhi
ya wazee wakiwa wameshika Silaha za Jadi walizotumia mababu zetu
kupigania dhidi ya kupinga utawala wa Wakoloni wa Kijerumani
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akiweka Sime.
Mpiganaji wa vita kuu ya pili ya Dunia Mzee Komba akisindikizwa na kamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenda kuweka shahada ya uwa katika mnala wa mashujaa.
Hii ni kwa nje ndivyo hali ilivyokuwa
Mhe
Balozi Hamisi Kagasheki(MB)Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na
viongozi wengine wakitoa salamu ya heshima kwa mashujaa wa majimaji
Hapo wanajeshi wakiendelea kutoasalamuza maombelezi kwa njia ya kijeshi
Kuinamisha kichwa chini ni dalili ya kumwomba mwenyezi Mungu awaweke Mahali pema Mashujaa walioo tangulia Mbele zahaki
Katika
kuwakumbuka Mashujaa waliotangulia mbele za Haki Jeshi la Wananchi
limeweka Utaratibu Maalumu ikiwa ni pamoja na kulipua mizinga na Fataki
katika kuwakenzi Mashujaa.
Jeshi la Wananchi wa Tanzania likitoka nje ya Uwanja wa Mashujaa baada ya kumaliza taratibu zote za Maombolezo.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mzuri na wakuelimisha juu ya vita vya majimaji.
Moja ya wageni waliohudhuria toka mikoa mbalimbali pamoja na nchi jilani ya Mozambiq
Chief Emanuel Zulu akiweka shada katika kaburi la pamoja la mashujaa wa vita vya majimaji.
Hili ndilo Kaburi la halaiki walipozikwa mashujaa wa vita vya Maji Maji , watu waliozikwa hapa ni 66
Eneo hili walilozikwa mashujaa hawa limekuwa eneo muhimu.
Mhe.Balozi Hamisi Kagasheki akipewa maelezo juu ya Kaburi la Songea Mbano ambaye alizikwa peke yake na jina la Mji wa Songea limetokana na jina lake
Balthazar Nyamusya Mhifadhi Kiongozi wa Makumbusho Ya Taifa Maji Maji Sonhgea akitoa maelezo kwa Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) alipokuwa
akizuru ukumbi wa historia ya vita vya maji maji.Miongoni mwa
vionyeshwa katika ukumbi wa historia ni zawadi iliyokabidhiwa na
MeyaAugusto Assique wa Jimbo la Lichinga kwa kutambua mashirikiano ya
kihistia na kitamaduni. Picha zote na Hamza Mashole
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)