Rais Dkt. Jakaya Kikwete juu akiweka shada la maua kwenye jeneza na kutoa heshima zake za mwisho. Chini kabisa akiwa na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakiweka udongo kwenye kaburi la Mzee Amos Kaguta wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura. Kulia ni Mama Janet Museveni
.....................................................
.....................................................
Picha na habari na Freddy Maro
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana aliungana na mamia ya wananchi wa
Uganda katika kushiriki Mazishi ya Mzee Amos Kaguta(97) Baba ya Rais
Yoweri Museveni wa Uganda,yaliyofanyika katika kijiji cha
Rwakitura,magharibi ya Uganda.
Rais
Kikwete aliwasili katika mazishi hayo akitokea Addis Ababa mji Mkuu wa
Ethiopia alipokuwa huko kuhudhuria Mkutano wa viongozi wa cnhi za Maziwa
Makuu uliokuwa na lengo la kutafuta amani ya kudumu katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo.
Akitoa
salamu zake za RambiRambi katika msiba huo Rais Kikwete alisema kuwa
Watanzania wapo pamoja na ndugu zao wa Uganda wakati huu wa majonzi na
kusema kuwa yeye binafsi anampa pole Rais Museveni na familia yake na
kumtaka awe na moyo wa subira katika kipindi hichi na kumuombea
marehemu.
Rais
Museveni alimshukuru Rais Kikwete kwa kufika katika msiba huo ambapo
alisema kuwa Marehemu Mzee Amos atakumbukwa kwa kuthamini elimu ambapo
aliwapeleka watoto wake shule na kwa kufanya mabadiliko ambapo alikubali
kufuata njia bora za ufugaji wenye tija jambo ambalo ni gumu kwa wazee
wengi wenye umri wake.
Rais
Museveni alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwatunza vyema wazazi wao
ili waishi muda mrefu na kulaani tabia ya baadhi ya vijana kuishi kwa
kutegemea mali za wazazi wao badala ya kuzalisha mali yao wenyewe
akiongeza kuwa wazee wana hazina kubwa ya maarifa kutokana na kukumbana
na changamoto nyingi katika maisha yao.
Marehemu Mzee Amos Kaguta alizaliwa mwaka 1916 katika kijiji cha Kabahambi,Kikoni Mtungamo nchini Uganda. Rais Kikwete na ujumbe wake akiwemo Waziri wa Ulinzi Mh.Shamsi Vuai
Nahodha waliondoka kurejea jijini Dar es Salaam baada ya mazishi hayo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)