Wadau kibao wajitokeza Kuona Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ulioonyeshwa na DStv kwenye Kiota cha Samaki Samaki Mlimani city jijini Dar - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Wadau kibao wajitokeza Kuona Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ulioonyeshwa na DStv kwenye Kiota cha Samaki Samaki Mlimani city jijini Dar

 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Multichoice Tanzania ambao ni wasambazaji wakuu wa Ving'amuzi vya DStv,Salum Salum (kulia) akizungumza na Wapenzi wa soka walikuwa wamefurika kwa wingi kwenye kiota cha Samaki Samaki,Mlimani City jijini Dar es Salaam jioni ya leo kwa kushuhudia Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (yanayofanyika huko nchini Afrika ya Kusini),ambapo DStv waliendesha zoezi hilo na pia kuchezesha bahati nasibu kwa wapenzi hao wa Soka walikuwepo hapo.Kushoto ni Meneja Mahusiano wa Multichoice Tanzania,Barbara Kambogi
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Multichoice Tanzania,Salum Salum na Meneja Mahusiano wa kampuni hiyo,Barbara Kambogi wakichezesha droo ya bahati nasibu ya Shinda King'amuzi cha DStv katika kipindi hiki cha Mashindano ya Kombe la Afrika.
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania,Barbara Kambogi (kushoto) akikabidhi King'amuzi hicho kwa Mshindi wa bahati nasibu hiyo,ambaye ni Mwanalibeneke wa Libeneke la Mtaa kwa Mtaa Blog,Othman Michuzi (pili kulia) mara baada ya kuibuka kidedea.(Duuhh.....!! jamaa anazali huyu!).
Baadhi ya Wadau wa DStv wakifuatilia Mtanange wa Ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika,kati ya timu ya Cape Verde na Afrika ya Kusini ambao ulimalizika kwa kutoka suluhu ya bila kufungana.
Wadau kibao toka maeneo mbali mbali ya jiji la Dar wakiwa kwenye Kiota cha Samaki Samaki jijini Dar kufuatilia Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika uliokuwa ukirushwa moja kwa moja kupitia DStv kutokea nchini Afrika ya Kusini yanakofanyika Mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages