UBALOZI WA JAPAN KUTIA SAINI MSAADA WA SHILINGI MILIONI 380 ZA UJENZI WA BWENI LINDI NA SHULE YA WALEMAVU MTWARA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

UBALOZI WA JAPAN KUTIA SAINI MSAADA WA SHILINGI MILIONI 380 ZA UJENZI WA BWENI LINDI NA SHULE YA WALEMAVU MTWARA

Balozi wa Japan Mr. Masaki Akodo
 
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada kesho anataraji kutia saini makubalino ya msaada wa fedha kiasi cha shilingi Milioni 380 kwaajili ya miradi miwili ya ujenzi wa bweni La Wasichana pamoja na Shule ya watoto wenye ulemavu katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Ubalozi huo jijini Dar es Salaam, inasemakuwa miradi hiyo ni upanuzi wa shule ya wenye ulemavu Dinyecha Wilayani Mtwara utakao gharimu zaidi ya shilingi Milioni 192 na ujenzi wa bweni la wasichana sekondari ya Ngapa ya Lindi utakaogharimu shilingi Milioni  188.

Miradi hiyo miwili inasimamiwa na taasisi za Tanzania Life Improvement  Association (TALIA) ya Mtwara na Women in Social Entrepreneurship (WISE) ya mjini Lindi.

Ubalozi wa Japan nchini Tanzania umekuwa ukichangia fedha katika miradi mbalimbali ya Maendeleo katika sekta ya Afya, elimu na maji tangu mwaka 1991 ambapo katika kipindi cha miaka 5 iliyopita mikoa ya Lindi na Mtwara imepatiwa msaada katika miradi 71 iliyogharimu dola za kimarekani 6,135,418 sawa na shilingi Bilioni 9,614,629485.

Utiaji saini huo utafanyika katika ofisi za mkuu wa Mkoa wa Lindi na Mtwara kati ya saa 3 asubuhi na saa 5.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages