Taswira zaidi Za Maadamano ya Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Kupinga mauaji ya Mwandishi Daudi Mwangosi - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Taswira zaidi Za Maadamano ya Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Kupinga mauaji ya Mwandishi Daudi Mwangosi

 Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Nevile Meena akihutubia katika mkutano uliofanyika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam jana, kulaani ktendo cha Polisi kumuua kwa bomu Mwandishi wa habari wa Kituoc ha Televisheni cha Channel Ten, Mkoa wa Iringa, marehemu Daudi Mwangosi katika vurumai zilizotokea wakati Chadema wakifungua tawi katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi hivi karibuni.
 Huyu ni Manyerere Jackton na bango lake
  Hili ni moja ya mabango waliyokuwa nayo waandishi
 Jese Kwayi, Mzee Maro na mwezake wakiwa kwenye maandamano hayo
 " Dk. Nchimbi ondokaaaaa" mwandishi akipaza sauti kuungana na wenzake waliokuwa wanamkataa kuwepo Kwa waziri wa mambo ya ndani Dk Emmanuel Nchimbi
  Mwandishi Lauden Mwambona akiwa amefunga mdomo kama hivi wakati wa maandamano hayo
  Hawa nao wakati mmoja ameziba mdomo, mwenzake akaziba macho kufikisha ujumbe wa kulaani mauaji ya Mwangosi
 Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi akiingia kwenye mkutano  wa wanahabari  viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam leo, walioandamana kupinga mauaji ya mwandishi mwenzao, Daudi Mwangosi wa Channel Ten Tv,
 Waziri wa Mambo ya Ndani Dk.Emmanuarl Nchimbi akajaribu kuwatuliza... waandishi bila mafanikio amabao walimtaka aondoke haraka enepo hilo
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk.Emmanuarl Nchimbi akiondoka akisindikizwa na viongozi wa Jujwaa la Wahariri
 Waandishi wakiingia viwanja vya Jangwani.Picha zote na Mdau Richard Mwaikenda na  Bashir Nkromo

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages