MKUU WA MKOA WA RUKWA AONANA NA UONGOZI WA TBL UNAOTAKA KUWEKEZA KWENYE ZAO LA SHAIRI MKOANI RUKWA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

MKUU WA MKOA WA RUKWA AONANA NA UONGOZI WA TBL UNAOTAKA KUWEKEZA KWENYE ZAO LA SHAIRI MKOANI RUKWA

 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na uongozi wa Kiwanda cha Bia cha Tanzania (TBL) uliomtembelea ofisini kwake leo ukiwa na lengo la kuwekeza kwenye kilimo cha shairi ambayo ni malighafi muhimu katika kiwanda hicho cha kutengeneza bia nchini. Mkoa wa Rukwa una ardhi yenye rutuba kustawisha mazao mbalimbali ya kilimo ikiwemo mchele, mahindi, maharagwe, ngano, alizeti, mtama, ulezi n.k. Katika kuwekeza kwao wataanza kwa kushirikiana na wakulima wadogowadogo ambao wapo Mkoani Rukwa kwa kuwawezesha zana bora za kilimo hicho pamoja na pembejeo ambapo pia watamiliki mashamba yao wenyewe kwa ajili ya kilimo hicho.

 Ndugu Gerry Van Den Houten ambaye ni Mkurugenzi wa Usambazaji wa Sabmiller ya South Africa ambayo ina mashirikiano na TBL akielezea lengo na faida za uwekezaji huo ambao licha faida kubwa itakayopatikana pia itatoa ajira kwa vijana wengi Mkoani Rukwa pamoja na kuhamasisha kilimo cha zao hilo. Kulia kwake ni Bennie Basson ambaye ni Menenja wa Shairi wa kiwanda hicho cha bia cha Tanzania (TBL). 
Timu ya Uongozi wa TBL ambayo pia ilikuwa imeongozana na baadhi ya wakulima wadogowadogo wa shairi Mkoani Rukwa wakiwa Ofsini kwa Mkuu wa Mkoa huo kwenye mazungumzo juu ya uwekezaji huo.Picha ya Pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, baadhi ya viongozi wa Mkoa na Viongozi wa TBL uliombatana na baadhi ya wakulima wadogowadogo wa shairi Mkoani Rukwa. (Picha na Hamza Temba-Rukwareviw blog-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages