Mkurugenzi
msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira,Bw. Richard Muyungi,
akifuatilia kwa makini mjadala unaeendelea katika mkutano wa kimataifa
wa mabadiliko ya tabianchi unaoendelea mjini Bangkok.
Katikati
ni Afisa mwanasheria kutoka ofisi ya makamu wa Rais Bi Margareth
Meela, akifuatilia majadiliano ya masuala ya mkataba wa Kyoto (KP)
katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi unaoendela mjini
Bangkok. kushoto kwake ni muwakilishi kutoka Uingereza na kulia kwake
ni muwakilishi kutoka Nchini marekani .
NA Evelyn Mkokoi, BANGKOK
Mkutano
wa mwisho wa maandalizi kwa ajili ya Mkutano wa 18 wa Nchi wanachama
wa Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika mwishoni mwa mwaka
huu huko Doha Qatar, umeanza leo hapa mjini Bangkok, Thailand.
Mkutano
huu unahusisha nchi zote wanachama kwa ngazi ya watalaamu, ili
kukubaliana masuala yote ambayo yatahitaji kuamriwa na mawaziri au wakuu
wan chi huko Doha. Masuala muhimu yanayojadiliwa ni pamoja na;
makubaliano kuhusu jinsi ya kushiirkisha nchi zote duniani kupunguza
uzalishaji wa gesi joto zinazosabisha kungezeka kwa joto la dunia.
Kwa
sasa joto la dunia limeongezeka kwa nyuzi joto zipatazo 0.8 kwa
takriban miaka mia moja iliyopita, na kwa kuwa sasa gesijoto
zinaongezeka sana inasadikiwa kuwa joto linaweza kuongezeka zaidi ya
nyuzi joto mbili kwa miaka hamsini ijayo kama nchi, hasa zile
zilizoendelea, hazitafanya juhudi za makusudi za kupunguza uzalishaji
wa gesitoto.
Majadiliano
haya yanaonekana kuwa magumu kwa sababu, upunguzaji wa gesijoto unagusa
uchumi wa nchi zilizoendea hasa katika sekta za viwanda, nishati na
usafirishaji; sekta ambazo zinazalisha gesi hizi kwa wingi, Pamoja na
hayo, Mkutano huu utazungumzia na kukubaliana pia kuhusu mambo mbali
mbali yaliyobaki kama kiporo katika mkutano wa Bonn ikiwa ni pamoja na
masuala ya misitu, jinsi ya kuongeza juhudi za kukabilana na athari za
mabadiliko ya tabinachi na upatikanaji wa fedha kukabilana na athari
hizi.
Akizungumza
katika ufunguzi wa mkutano huu, Bwana Richard Muyungi, Mkurugenzi
Msaidizi, Ofisi ya Makamu wa Rais, ambyae ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Dunia ya Sayansi na Teknologia ya Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi
na pia Makamu wa Rais wa Mkataba akiiwakilisha Afrika, alisema Afrika
ikiwa ni pamoja na nchi kama Tanzania ina matumani makubwa kuwa nchi
zote dunaini na hasa zilizoendelea ya kufanya juhudi za makusudi za
kupunguza gesijoto ili dunia iwe salama.
Pamoja
na juhudi hizi alisistiza haja ya kuzisaidia nchi ambazo tayari
zinakabiliwa na athari kubwa kupewa msaada wa fedha na utaalamu
kukabiliana na athari hizi. Alisema,msaada huu usiwe mkopo kwani ni
wajibu wanchi ambazo zimesababisha tatatizo hili kulinda haki ya kuishi
na kuwa na maendeleo yanayotakiwa kwa nchi nyingi za Afrika amabazo
hazikusababisha tatatizo hili lakini zina uwezo mdogo wa kiuchumi
kukabiloana na madhara haya makubwa, kitolea mfano wa athari mbali
mbalia ambazo tayari zimejitokeza Tanzania, ikiwa ni pamoja na madhara
makubwa yanayosababishwa kuongezeka kwa kina cha bahari kwa maeneo ya
pwani mwa Tanzania na Zanzibar.
Akiongea
kwa kofia ya Makamu wa Rais kwa niamba ya Afrika, ameongeza kuwa, suala
la matumizi ya nishati ya mafuta kwenye sekta ya viwanda, usafiri na
usafirishaji litabakia kuwa muhimu hadi nchi nyingi zinazoendeea hasa
za Afrika zitakaposaidiwa kupata nishati mbadala, zitakazokuwa endelevu
na kwa bei nafuu. Pamoja na nia njema ya nchi hizi kutaka
kushirikiana katika kupunguza gesijoto, uchumi wanchi nyingi maskini
utaendelea kutegemea nishati ya mafuta na makaa ya mawe kwani ndiyo
inayoweza kupatika kwa urahisi zaidi katika kujiletea maendelo endelevu
kwa sasa.
Wakati huo huo,
akifungua Mkutano huu, Mkurugenzi Mkuu wa ‘Secretariat’ ya Mkataba huu,
Bi Christiana Figueres, alihimiza nchi zote zilikubali kufanya kazi
kwa kushirikiana kwa karibu na uwazi katika kukabilana na tatatizo hili
, na mataifa yote yatambue umuhimu wa kuhakikisha upatikanaji wa
fedha kwa ajili ya kuzisaidia nchi zinazoedelea katika kuhimili na
kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha
nchi nyingi zilizoendelea zilizozungumza zilisistiza haja ya kuheshimu
Makubaliano yaliyo katika mkataba na hasa misingi muhimu iliyowekwa
kwa kutambua kuwa kuna nchi zenye wajibu wa msingi wa kutataz tatizo
hili.
Ujumbe
wa Tanzania unaowakilisha katika mkutano huu, unashirkisha pia
Wawakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, na
wataalamu wengine kutoka Ofsis ya makamu wa Rais mazingira.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)