Matumla akisulubiwa jukwaani wakati wa mpambano huo.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Juma Kassim ‘Juma Nature’, akionyesha ukongwe wake.
Kiongozi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf akiwapagawisha mashabiki zake.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Estelinah Sanga ‘Linah’, akiwa jukwaani.
Mwasiti Almasi akikamua na wacheza shoo wake.
Maunda Zorro akionyesha umaarufu wake.
Sadick Momba (kushoto), akipambana na Venance Mponji katika mpambano wa utangulizi ambapo Sadick aliibuka mshindi.
Julius Thomas (kushoto),
akizidunda na Jumanne Kirumbe kabla ya Maneno Oswald na Matumla kupanda
ulingoni. Julius alishinda mpambano huo.
Mmoja wa wasanii wa kundi la Mabaga Fresh ambaye sasa yuko katika kundi la Wanaume Halisi, JB Mkuu wa Maadui akiwajibika.
Malkia wa Bendi ya Jahazi Modern Taarab, Leila Rashid akiwajibika.
Watoto wakicheza muziki ndani ya bwawa la kuogelea.
Baadhi ya umati uliokuwa ndani ya ukumbi huo.
Bondia Maneno Oswald akitangazwa baada ya kumdunda Rashid Matumla.
..............................................
MPAMBANO wa ndondi baina ya
mabondia Maneno Oswald na Rashid Matumla ambao ulifanyika ukumbi wa
maraha wa Dar Live Mbagala, jijini Dar es Salaam, katika kuadhimisha
sikukuu ya Idd el Fitr, ulishuhudia Oswald akimchakaza Matumla kwa
pointi.
Mbali na mpambano huo uliofanyika
usiku wa kuamkia leo, kulikuwa pia na burudani za aina mbalimbali,
likiwemo disko la watoto ambao pia walifurahia kuogelea katika bwawa
maalum na michezo mingine mingi. Kwa upande wa muziki kulikuwa na shoo
kali zilizofanywa na wanamuziki Juma Nature, Mwasiti Almasi, Estelinah
Sanga ‘Linah’, Maunda Zorro na kundi zima la Jahazi Modern Taarab
likiongozwa na mfalme, Mzee Yusuf. Picha: Musa Mateja na Richard Bukos/GPL.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)