Mchezaji wa timu ya Yanga Stefano Mwasika akikokota mpira kuelekea goli
la timu ya Mafunzo ya Zanzibar huku beki wa timu ya Mafunzo Ismail
Khamis Amour wakati timu hizo zikichuana katika mchezo wa Robo Fainali
ya Kombe la Kagame unaofanyika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa, mpira
umekwisha na timu ya Yanga imeshinda kwa penati 5-3 baada ya kutoka
suluhu katika kipindi cha dakika tisini za mchezo huo, magoli 1-1 ambapo
timu ya Mafunzo ilijipatia goli lake kupitia mchezaji Ali Othman Mpemba
katika dakika ya 35 kipindi cha kwanza huku lile la Yanga likifungwa
na Said Bahanuzi katika dakika ya 46 kipindi cha pili, ndipo baada ya
dakika tisini penati zikapigwa Yanga kufanikiwa kuifunga Mafunzo kwa
matuta
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)