Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck
Sadiki (katikati) akiongea na waandishi wa habari Katika viwanja vya
Mnazi mmoja leo jijini Dar es Salaam kueleza namna mkoa ulivyojipanga
kufanikisha sherehe za maadhimisho ya siku ya mashujaa itakayofanyika kitaifa tarehe 25, Julai 2012 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam
Askari
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakitoa heshima kwenye mnara wa
kumbukumbu ya Mashujaa katika viwanja vya mnazi mmoja leo ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya
mashujaa.
Askari
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) watakaoshiriki kwenye gwaride
wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa wakiendelea na mazoezi katika
viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Kiongozi wa mabalozi wa nchi za Afrika wanaoishi nchini Tanzania Balozi Ibrahim Mukubi kutoka Uganda
akiweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa leo jijini
Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe ya siku ya
mashujaa itakayofanyika tarehe 25, Julai 2012.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO. Dar es salaam.
Wananchi
wa mkoa wa Dar es salaam wameombwa kujitokeza kwa wingi wakati wa
sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa itakayofanyika
kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja tarehe 25 Julai 2012 jijini Dar
es salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam , Mkuu wa mkoa wa Dar
es salaam Saidi Meck Sadiki amesema maandalizi ya maadhimisho hayo
yamekamilika na kufafanua kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo atakuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
Amesema katika maadhimisho hayo kwa upande wa mkoa wa Dar es salaam baadhi ya barabara zitafungwa
ikiwemo barabara ya Nyerere, Uhuru na Bibi Titi Mohamed ili kuhakikisha
usalama kwa wale wote watakaohudhuria maadhimisho hayo na kuongeza kuwa
katika kuboresha maadhimisho hayo kamati ya maadhimisho itaweka luninga
katika maeneo yote muhimu ili kuwawezesha wananchi kuona yanayotendeka
wakati wa maadhimisho hayo.
Aidha
Bw. Meck Sadiki amesema kuwa maadhimisho hayo ni kumbukumbu muhimu
katika historia ya Tanzania kwa kuwaenzi mashujaa waliojitoa muhanga
katika jitihada za kuikomboa na kuilinda Tanzania.
“
Maadhimisho haya ni kumbukumbu muhimu sana katika historia ya nchi yetu
kwani tunawaenzi mashujaa wetu waliojitoa muhanga katika jitihada za
kuikomboa, kuilinda na kudumisha amani na utulivu wan chi yetu”
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)