WAKIMBIZI WA KITANZANIA WAREJESHWA NCHINI KWA NDEGE YA UMOJA WA MATAIFA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

WAKIMBIZI WA KITANZANIA WAREJESHWA NCHINI KWA NDEGE YA UMOJA WA MATAIFA

 Watanzania waliokuwa wakiishi ukimbizini Mogadishu Somalia wakirejea nchini jana na ndege ya Umoja wa Mataifa wakiwa na familia zao walikokuwa wakiishi tangu Januari 2001 wakikimbia vurugu zilizotokea Zanzibar baada ya Uchaguzi Mkuu, Watanzania hao ni 38 wakiwa pamoja na wake zao, Raia wa Somalia pamoja na watoto
 Baadhi ya Wanzania 38 waliokuwa wakimbizi Jijini Mogadishu wakielekea sehemu ya mapokezi mara baada ya kushuka katika ndege la Umoja wa Mataifa iliyowaleta nyumbani wakiwa na wake zao walioa nchini Somalia baada ya kuishi huko kwa miaka 11,walikimbia vurugu za Januari 26/27 mwaka 2001
  Baadhi ya Watanzania waliokimbilia Mogadishu mwaka 2001 wakiwa katika Ofisi ya Uhamiaji Zanzibar jana. Wa kwanza ni Mohammed Adam(38)  akiwa amembeba mwanawe mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume,wanaotazama kamera ni baadhi ya wake wa Watanzania hao ambao ni raia wa Somalia waliowasili jana wakitokea Mogadishu Somalia na ndege ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia huduma za kibinadamu
 Baadhi ya Watoto wakiwa na wazazi wao Raia wa Tanzania waliokuwa wakimbizi nchini Somalia wakiwa katika Ofisia za Uhamiaji uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mara baada ya kuwasili na ndege la UN zinazohusika na huduma za kibinadamu.
 Baadhi ya akinamama Raia wa Somalia ambao wameolewa na Watanzania waliokuwa ukimbizini Mogadishu wakifurahia jambo walipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume,hapa walikuwa wakisubiri taratibu za Uhamiaji
 Watoto ambao kwa sasa ni Raia wa Somalia wakiwa na wazazi wao Raia wa Tanzania waliokuwa wakimbizi nchini Somalia wakisubiri taratibu za Uhamiaji katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume jana baada ya kuwasili wakitokea Mogadishu na ndege ya Umoja wa Mataifa chini uangalizi wa UNHCR
Watanzania waliokuwa wakimbizi katika kambi ya Mogadishu wakielekea kupanda mabasi maalum yaliyoandaliwa na Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume jana(Picha na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages