SHABIKI WA SIMBA AJISHINDIA PIKIPIKI KATIKA BAHATI NASIBU YA 'FAN SIMBA' - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

SHABIKI WA SIMBA AJISHINDIA PIKIPIKI KATIKA BAHATI NASIBU YA 'FAN SIMBA'


Ofisa habari wa mabingwa wa soka wa Tanzania, Simba SC, Ezekiel Kamwaga (kulia) akimkabidhi  funguo ya Pikipiki Shabiki wa timu hiyo, Abubakari Hamis (katikati) kutoka Arusha baada ya kuibuka mshindi katika bahati nasibu ya Simba Fan Club katika hafla fupi  iliyofanyika jijini Dar es Salaam, jana. Kushoto ni Meneja wa kampeni hiyo, Talib Rashid, kutoka kampuni ya Push Media Moobile. Washiriki wa bahati nasibu hiyo wanatakiwa kutuma neno Simba kwenda kwenye namba “15678” na kuingia katika droo.
************************************
Na Mwandishi wetu

KLABU ya Simba imewataka wapenzi na mashabiki wake kuendelea kujiunga na huduma ya kutuma ujumbe mfupi kupitia huduma ya Fan Simba Club ili kupata taarifa mbalimbali za Simba ikiwemo matokeo ya michuano ya kombe la Kagame  inayotarajia kuanza Julai 14 mwaka huu na masuala ya Usajili.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa mshindi wa Bahati Nasibu ya Fan Simba, Ofisa Habari wa Klabu hiyo Ezekiel Kamwaga alisema kupitia huduma hiyo mashabiki wa Simba watapokea taarifa  za kila siku  ambazo wao watakuwa wa kwanza kuzipata kupitia huduma hiyo.

Alisema pia itaisaidia klabu ya Simba kujiongezea mapato yatakayoiwezesha klabu hiyo kuendesha mambo yake katika ufanisi mkubwa ikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji wazuri.

Kwa upande wake Meneja  Kampeni wa Kampuni ya Push Mobile Talib Rashid ambao wameingia mkataba na klabu ya Simba kupitia huduma ya sms Fan Simba Club wamefunga droo ya bahati nasibu waliokuwa wakiichezesha kwa klabu ya Simba kupitia huduma hiyo kwa kutoa pikipiki na bajaji.

Bahati nasibu hiyo iliyokuwa ikichezwa kwa kipindi cha miezi mitatu sasa imefungwa kwa kuwapata washindi ambao ni wanafunzi wa shule za Sekondari huku mmoja akiwa ni Tito Zakaria kutoka shule ya Sekondari ya Mong'ola iliyopo Dodoma aliyejishindia pikipiki na Mohamed Ibrahim kutoka shule ya Sekondari ya Chandama iliyopo Kondoa na kujishindia bajaji.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages