Katika dunia ya leo, kuwa na website sio kitu cha kuchagua tena
bali ni cha lazima, ila kuwa website inayofanya kazi kwa gharama nafuu
ni chaguo madhubuti. Katika kulitambua hili, timu nzima ya AfroIT.com
inakuletea mafundisho ya kutengeneza website kwa kutumia award winning
open source Joomla bila gharama yoyote. Mafunzo haya yenye module 17
hadi sasa yameshafikia module ya kumi.
Mafunzo
haya yanayotolewa kwa kiswahili tena kwa mtindo wenye uhalisia wa
Mtanzania, yanawafaa watu wote kuanzia mtengeneza tovuti, mmiliki wa
blog nk, hivyo wakati ni huu sasa.
Unaweza kuangalia mafunzo haya kwenye Youtube Channel yetu au moja kwa moja toka kwenye tovuti yetu ya AfroIT.com. Pia unaweza kudownload na kuweka kwenye simu, kompyuta, iPad nk na ukawa unapata mdidi kila ulipo.
Pia usisite kutumia Forums kwa ajili ya majadiliano pindi unapopata utata kwenye mafunzo na kuhitaji msaada.
The Team
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)