Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akiweka Ngao na
Mkuki kwenye Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya siku ya
kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam, leo.
Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange akitoka kuweka silaha ya jadi
kwenye Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu
ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam, leo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiwasili
kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo, kuhudhuria
sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, leo.
Kutoka
(kushoto) Rais Dkt. Jakaya Kikwete, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa pili wa Rais
wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan
Mwinyi, Spika
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho....., Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Mkoa wa
Dar es salaam, Said Meck Sadiq, wakiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakihudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, leo.
Sehemu ya wageni waalikwa na Mabalozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo.
Askari wa Jeshi wakishiriki katika maadhimisho hayo, hapa wakiweka silaha begani.
Ni ishara ya kutoa heshima kwa Mashujaa wapiganaji.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete, akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita
mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika
maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye
Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita mbalimbali vya
ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku
ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam, leo.
Huyu
ni Mzee CUF, ni maarufu kwa upigaji picha za kuuza 'BANYAA' huyu pia ni
miongoni mwa wapiganaji ambao walipata kupigania haki ya Mtanzania wa
leo enzi hizo, ambaye kwa sasa kazi yake kubwa ni kujishughulisha na
uuzaji wa picha katika shughuli mbalimbali, hapa akihaha kusaka matukio
ya kuweka katika karatasi ya picha zake ambazo baadaye atafanya
biashara. Mzee huyu baada ya kuona siku ya leo ni muhimu hata kwake pia
lakini akiweka kazi yake mbele zaidi ili kujipatika kipato alionelea ni
vyema naye pia akakumbukia mavazi yake haya aliyoyavaa na kutinga nayo
eneo la tukio ili kuepuka kusumbuliwa na wahusika aweze kuingia kirahisi
eneo la tukio kama unavyomuona akiwa bize na vazi lake huku akiwa na
begi kubwa la kamera wakati kajikamera alikonako ni kibiriti. Hii yote
ni janja tu ilimradi mkono uende kimiani.
Mzee
CUF, akiwa bize kunasa picha za wajeda wakiwa katika paredi, begani ni
bonge la begi la kamera ambalo ndani yake halina kilichokusudwa.
Mzee CUF bado yu bize........
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akiomba dua kwa niaba ya waislam wakati wa maadhimisho hayo leo.
Kiongozi wa dini ya kikristo, Mchungaji Kamoyo, akiomba sala kwa niaba ya wakristo wakati wa maadhimisho hayo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, wakati akiondoka
kwenye uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo baada ya
kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)