MASHALI V/S SAMSON ULINGONI-Friends corner hotel jumapil - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

MASHALI V/S SAMSON ULINGONI-Friends corner hotel jumapil


Mabondia Thomas Mashali na Maisha Samson wamemaliza zoezi zima la upimaji na tayari kwa ajili ya mpambano wao utakao fanyika katika ukumbi wa Friends corner hotel-manzese siku ya jumapili 24/6/2012. mpambano huo wa ubingwa wa taifa wa TPBO uzito wa midle na unaosimamiwa na TPBO chini ya rais wake Yasin Abdallah na katibu mkuu Ibrahim Kamwe umemalizika vizuri na mabondia wote wapo katika hali nzuri na tayari kwa fight.
 
Zoezi zima la upimaji lilisimamiwa na Ibrahim kamwe na kueleza kuwa mabondia hao wote wawili kwa pamoja wamepata @kilo 71 na watacheza raundi kumi.

pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi kama ifuatavyo;


juma fundi(52kg) v/s shaban madilu (49.5kg) - watacheza raundi nane mohamed shaban'ndonga' (61kg) vs Musa hassan (61kgs) - watacheza raundi sita Jonas godfrey (61.5kgs) vs Venance mponji(59kg) - watacheza raundi sita Abdalah mohamed'prince naseem'(64kgs) vs Yohana Mathayo(65.5kgs)- raundi sita Nasoro Hatibu 55kg vs Abdul Athuman 55kgs -watacheza raundi nne

Martin Richard 50kgs vs Hassan Kadenge 49kgs -watacheza raundi nne

ngumi zitaanza kama kawaida kuanzia saa kumi jioni, na tunarudia tena kusema katika ngumi hakuna kupendelea na TPBO itasimamia kwa haki zote bila kuangalia mtu. tutakachoangalia ni mchezo kuchezwa kwa kanuni za ngumi na utoaji points kulingana na bondia anavyoscore kwa ngumi
  halali sio kulingana na makelele ya washabiki .

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages