Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad Atembelea Chemchem ya Mtopepo Zanzibar - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad Atembelea Chemchem ya Mtopepo Zanzibar

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk. Mustafa Ali Garu, akimuonesha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad namna chemchem inavyotiririka, katika chemchem ya Mtopepo walipofanya ziara ya kutembelea chemchem hiyo jana tarehe 19/06/2012.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na uongozi wa ZAWA wakiangalia upungufu wa maji katika eneo la Mtopepo alipofanya ziara ya kutembelea chemchem ya Mtopepo jana. Kuliani kwake ni Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Mhe. Ramadhan Abdallah Shaaban.Picha na Salmin Said-Ofisi Ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
---
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema serikali italazimika kutumia ukali na kuondoa muhali kwa watu wanaoendeleza vitendo vya uchafuzi wa mazingira hasa katika vianzio vya maji. 

 Amesema ni hatari kuona vitendo hivyo vikiendelea huku taifa likikabiliwa na uhaba wa maji unaotokana na uharibifu wa mazingira katika vianzio hivyo. 
Akiwa katika ziara ya kutembelea vianzio vya maji katika chemchem ya Mtopepo, Maalim Seif ametahadharisha kuwa ikiwa vitendo hivyo vitaachiwa kuendelea, kuna hatari ya taifa kuwa na upungufu mkubwa wa maji katika miaka michache ijayo.

 “Inabidi sasa tuwe wakali ili isije ikafika wakati tukawa hatuna maji katika nchi yetu”, alitahadharisha Maalim Seif. 

 Amesema katika kudhibiti hali hiyo, serikali itachukua kila aina ya tahadhari kuhakikisha kuwa vianzio vya maji haviendelei kuharibiwa kwa maslahi ya vizazi vijavyo na taifa kwa ujumla.

 Akizungumza katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) Dk. Mustafa Ali Garu amesema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo kwa sasa ni uvamizi wa ujenzi karibu na vianzio vya maji, hali inayopelekea mfumo wa uzalishaji wa maji kubadilika na kupunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha maji katika chemchem. 

 Kwa upande wake Mhandisi wa Mamlaka hiyo injinia Said Saleh amesema baadhi ya chemchem ndogo ndogo zimeanza kutoweka, na kutaka tahadhari zaidi zichukuliwe katika kudhibiti uvamizi wa vianzio hivyo. 

Amefahamisha kuwa karibu nusu ya kiwango cha maji yamepungua katika kipindi cha miaka kumi iliyopita kutoka katika chemchem za Mtotopepo na Mwanyanya, huku chemchem ya Mtopepo ikiwa na upungufu mkubwa zaidi.Ziara hiyo pia imemshirikisha Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Mhe. Ramadhan Abdallah Shaaban
 
 
Na 
Na Hassan Hamad
Ofisi Ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages