Baraza la Sanaa (BASATA) lawapa somo waandaaji wa Epic Bongo Star Search 2012 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Baraza la Sanaa (BASATA) lawapa somo waandaaji wa Epic Bongo Star Search 2012


Na Mwandishi Wetu
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limeendesha semina ya siku moja kwa majaji wa shindano la Epic Bongo Star Search 2012 kwa kuwataka kuzingatia maadili ya kazi zao.
  Akitoa somo kwa majaji hao mratibu wa matukio wa Basata Malimi Mashili aliwataka majaji hao kutambua kuwa asilimia kubwa  ya washiriki wanategemea zaidi msaada wao katika kukuza vipaji.
 Mashili aliwataka majaji hao kutambua kuwa mazingira waliyotoka washiriki na kuangalia namna ya kuwasaidia kulingana na mikoa yao kwa kuwa wapo ambao wana vipaji lakini wanatatizwa na suala la kuyazoea mazingira.
  Alisema kuwa kwa kuwa mwaka huu EBSS itaruhusu washiriki wa miaka 16 hivyo ni vema zaidi wakazingatia suala la sauti kulingana na umri wa mshiriki sababu watakuwepo wenye sauti za kitoto pia.
  Pia aliwataka majaji hao kuhakikisha kuwa hawatoi aina yoyote ya upendeleo na wala kuwa karibu zaidi na baadhi ya washiriki wa shindano hilo.
  Pia alisisitiza kuwa majaji wanalo jukumu kubwa la kuwaelekeza namna ya kuimba, kuvaa, kujiheshimu na usafi wa mwili pia.
  “Hiii ni semina ya kuwekana sawa tu kwa kuwa hili shindano lipo kwa muda mrefu na majaji mmekuwa mkifanya vema, kwa niaba ya BASATA napenda kuchukua muda huu kuwataka muwe makini katika kuzingatia maadili haya niliyoyasema na hata mengine pia”alisema Mashili.Naye Mkurugenzi wa Berchmark Production inayoandaa shindano hilo Ritha Paulsen alisema kuwa semina hiyo ni muhimu kwa majaji kwa kuwa  muda mzuri wa kukumbushana mambo muhimu yahusuyo muziki.
  Epiq Bongo Star Search mwaka huu inaanzia mkoani Dodoma Juni 16 katika ukumbi wa Royal Village.
  Majaji wa shindano hilo waliohudhuria ni pamoja na Jaji Mkuu Ritha Paulsen, Master Jay, Salama  pamoja na mratibu wa EBSS kutoka Basata Vicky Temu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages