Rais Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa kuamkia leo May 20, 2012
alikaribisha kwa chakula cha jioni uongozi wa Jumuiya ya Watanzania
wanaoishi Washington na vitongoji vyake katika hoteli ya Ritz-Carlton
jijini Washington DC. Uongozi huo, kwa niaba ya wanachama wake,
ulimpongeza Rais Kikwete kwa kuwa mmoja wa Marais wanne wa Afrika
walioalikwa kwa mara ya kwanza katika historia kuhudhuria kikao cha nchi
tajiri duniani zijulikanazo kama G-8 katika makazi ya mapumziko ya Rais
wa Marekani ya Camp David, Maryland. Rais wa jumuiya hiyo Bw. Iddy
Sandaly alisema kwamba mualiko wa kuhuduhuria mkutano wa G-8 alioupata
Rais Kikwete umeendelea kudhihirisha kwamba mataifa makubwa yanaheshimu
msimamo wake katika kuendeleza kilimo cha kisasa na kuondoa njaa
duniani, ambavyo ndivyo vilivyokuwa kauli mbiu ya mkutano wa Camp David.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na waziri wa kilimo Injinia
Christopher Chiza pamoja na Waziri wa kilimo wa Zanzibar Mh Suleiman
Othman Nyanga, pamoja na balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh Mwanaidi
Sinare Maajar. (Picha na Ikulu)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)