Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (kushoto)
akibadilishana hati ya mkataba wa mkopo nafuu na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Waarabu
inayojishughulisha na Maendeleo ya Uchumi ya Afrika (BADEA) Bw. Abdelaziz
Khelef (kulia)leo mjini Arusha wa mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa
kilometa 22.1 kutoka Wete hadi Chakechake kisiwani Pemba. Mradi huo utagharimu
shilingi bilioni 15.
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (kushoto) akitoa
ufafanuzi kwa waandishi wa habari jana mjini Arusha mara baada ya kubadilishana
hati ya mkataba wa mkopo nafuu na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Waarabu inayojishughulisha
na Maendeleo ya Uchumi ya Afrika (BADEA) Bw. Abdelaziz Khelef (kulia) wa mradi
wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 22.1 kutoka Wete hadi Chakechake
kisiwani Pemba. Mradi huo utagharimu shilingi bilioni 15.
Waziri wa Fedha na Mipango Ofisi ya Rais Yusuf Omar
Mzee (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jana mjini Arusha juu
ya umuhimu wa barabara mpya inayotarajiwa kujengwa kutoka ChakeChake hadi Wete
kisiwani Pemba mara baada ya Tanzania na Benki ya Waarabu inayojishughulisha na
Maendeleo ya Uchumi ya Afrika (BADEA) kusaini mkataba wa mkopo wa masharti
nafuu wa mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 22.1. Kulia ni
Waziri wa Miundombinu ,Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Zanzibar Hamad Masoud
Naibu Waziri wa Fedha Saada Salum (katikakati) akibadilishana mawazo na Msemaji
wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma(kushoto) wakati wa mapumziko baada ya
mikutano mbalimabli inayoendelea mjini Arusha ya Benki ya Maendeleo ya
Afrika(AfDB). Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Zanzibar Amina
Khamis Shaaban.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)