Napenda
kutoa pongezi zangu kwa Mheshimiwa Kigoda kwa kuchaguliwa kuiongoza
wizara ambayo kwa sasa imekumbwa na kashfa nyingi sana hususan madudu ya
TBS.
Najua kwa uteuzi huu mheshimiwa Rais alifikiria sana na alimuona Kigoda kuwa ndie mtu anayefaa kuyasafishia mbali madudu haya.
Mheshimiwa Kigoda,
Kabla
hujaakaa vizuri kwenye kiti chako cha uwaziri baada ya kuapishwa
nakuomba kwanza ujiulize ni kitu gani hasa kilichomuondoa unayemrithi
hicho kiti?
Mie nitakusaidia kwa kukumbusha tu pamoja na kuwa najua unalielewa hilo fika.
Aliyekuwa hapo kabla yako anaitwa Mheshimiwa Chami ambaye sasa kazi yake ni mbunge, na kilichomtoa hapo ulipo wewe sasa ni yale madudu ya EKELEGE/TBS ambayo yametambaa kila kona ya hiyo ofisi.
Haya madudu usipoyaondoa basi ujue yataanza kukutambaa na wewe. Niliwahi kumuandikia Mheshimiwa Chami email nyingi ambazo najua alikuwa hata hazisomi na hata kama alizisoma basi alikuwa anadharau tu.
Wabunge walimshauri Chami amsimamishe kazi huyu Ekelege ili apishe uchunguzi lakini alikataa na kusema kufanya hivyo itakuwa ni kumnyima haki Ekelege.
Ripoti ya wabunge ilipelekwa kwa spika kuhusu madudu haya na spika aliipeleka kwa CAG ili ifanyiwe kazi lakini Chami kila kukicha alikuwa anasema hajaiona hiyo ripoti hivyo anaisubiri ikimfikia ndio atajua afanye nini.
Hii ilidhihirisha jinsi huyu bwana asivyo mchapa kazi. Yaani wewe tuhuma zote hizi nzito na ushahidi wote huu unaotolewa kwenye vyombo vya habari na wabunge wakisapotiwa na Mie mjumbe mwenye hasira kali pamoja na mwenyekiti wangu Mjengwa bado kaka ulikuwa huoni sababu ya kufanya lolote bali unakaa tuuuuu ofisini unataka CAG akufuate akupe report.
Mie nadhani kwa kiongozi bora kama vile Magufuli au Mrema enzi zake ungeinuka na kwenda mwenyewe kwa CAG kuomba kuiona hiyo ripoti. Kitendo cha kila siku kusema hujaiona hiyo ripoti wakati hata Naibu wako Nyalandu anakuambia umsimamishe kazi Ekelege ni uzembe wa hali ya juu na sidhani kama huyu mtu anafaa hata kuwa Mkuu wa Wilaya.
Kile kitendo cha kudharau ushauri wa wabunge ni kitendo cha kudharau Watanzania wote kwani wao ndio waliowachagua hao wabunge wakawawakilishe.
Turudi kwenye ushauri.
Mheshimiwa
Rais ameisha fanya kazi yake ambayo ni kumtoa mtu wa juu kabisa ambaye
ni Chami, sasa kinachotakiwa ni wewe Mheshimiwa Kigoda kumalizia kazi
aliyoianzisha Rais.
Kumbuka unapoua nyoka inabidi uponde ponde kichwa sio kukanyaga mkia. Haya madudu yalitokea kwa Ekelege na vimiradi vyake vya ukaguzi wa magari nje ya nchi ambapo kuna kampuni hewa huko Hongkong na na Uk ambapo kuna hiii kampuni ya WTM UTILITY ambayo yenyewe ndio duka kubwa la kuuza vyeti vya EKELEGE/TBS.
Hizi tenda zilitakiwa zilitolewe miaka mitano iliyopita na sasa huu mwezi wa tano ulitakiwa uwe ndio mwisho wa kuuza vyeti lakini inavyoonekana jamaa wameamua kuendelea mpaka hapo watakaposimamishwa na Serikali, lakini sio TBS kwa sababu TBS ndio wao.
Kumbuka unapoua nyoka inabidi uponde ponde kichwa sio kukanyaga mkia. Haya madudu yalitokea kwa Ekelege na vimiradi vyake vya ukaguzi wa magari nje ya nchi ambapo kuna kampuni hewa huko Hongkong na na Uk ambapo kuna hiii kampuni ya WTM UTILITY ambayo yenyewe ndio duka kubwa la kuuza vyeti vya EKELEGE/TBS.
Hizi tenda zilitakiwa zilitolewe miaka mitano iliyopita na sasa huu mwezi wa tano ulitakiwa uwe ndio mwisho wa kuuza vyeti lakini inavyoonekana jamaa wameamua kuendelea mpaka hapo watakaposimamishwa na Serikali, lakini sio TBS kwa sababu TBS ndio wao.
Mie nitakusaidia kusafisha haya madudu kwa kukupatia ushahidi nilionao bure na nitasafiri mpaka huko kwa nauli yangu ili nikupatie ushahidi mwingi nilionao ambao Chami aliupuuzia na sasa kibarua kimeota nyasi.
Kule Iringa kuna mti mmoja unaoitwa MKAYEWA au waswahili huuita mti wa kisamvu. Huu mti ukiukata baada ya wiki moja utakuta umeota tena kwa hiyo kama unataka kuuondoa kabisa inakubidi ung'oe kabisa huu mti na mizizi yake yote ili usiote tena.
Kwa kusema hivyo, nakushauri kuwa inabidi uwaondoe wote waliohusika na hizi tenda feki za ukaguzi wa magari kuanzia kwenye hivi vikampuni kama WTM mpaka kwa huyo mwenyewe EKELEGE ambaye Chami alimkumbatia sana na mwisho wake kang'olewa yeye.
Hebu jiulize , kwa nini uhatarishe kibarua chako kulinda watu ambao wamepewa dhamana ya kukagua magari badala yake wameamua kuuza vyeti vya TBS.
Mie sidhani hata kama kuna hela lakini sio nyingi za kumfanya mtu apoteze nafasi yake ya uwaziri. (mshahara wa waziri, marupurupu ya ubunge na heshima uliyopewa ni kubwa sana )
Mie nakuomba uipitie report ya CAG na uifuate mwenyewe au hata ukimtuma dereva lakini uipate uisome na uifanyie kazi, usikae chini kama jamaa yangu Chami ambaye alikuwa anatoa sababu ambazo najua yeye mwenye hapo alipo sasa akikaa nyumbani kwake anasema ningejua???? Ningemsikiliza mjumbe mwenye hasira kali kama sio akina Zito Kabwe na Filikunjombe.
Mwenyekiti Mjengwa
Nakuomba uufikishe huu ujumbe kwa Mheshimiwa Kigoda ili aufanyie kazi
Nakuomba umuwekee na hizi picha hapa juu ili zimpe taswira halisi ya haya madudu
Asante sana
MJUMBE MWENYE HASIRA KALI SANA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)