Mke
wa Waziri Mkuu Tunu Pinda pamoja na Kaimu Katibu Mkuu wa Chaneta Rose
Mkissi wakipokea vifaa vya michezo kwa ajili ya timu ya taifa ya
Netiboli- Taifa Queens kutoka kwa Meneja wa Mahusiano ya
Nje wa Vodacom Bw. Salum Mwalim. Vodacom imeipatia Taifa Queens vifaa
mbalimbali vyenye thamani ya Shilingi Milioni Sita kuwezesha ushiriki
mzuri wa timu hiyo kwenye mashindano ya Afrika yanayoanza kesho
(Jumanne Mei 8, 2012) jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia ni mjumbe
wa kamati ya maandalizi ya mashindano Shiza Mwakatundu
--
Kamapuni
ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania leo imeipiga jeki timu ya taifa
ya Netiboli - Taifa Queens kwa kuipatia vifaa mbalimbali vya michezo
vyenye thamani ya shilingi milioni sita kuiwezesha timu hiyo kushiriki
vema mashindano ya Afrika yanayoanza kesho jijini Dar es salaam.
Vifaa
hivyo ni suti za michezo jozi 20, viatu vya michezo jozi 20, jezi seti
mbili, BiBs 20 vyote vikiwa na thamani ya Sh. Milioni Sita na
kukabidhiwa leo kwa Mke wa Waziri Mkuu Tunu Pinda kutoka kwa Meneja wa
Mahusiano ya Nje wa Vodacom Tanzania Bw Salum Mwalim katika hafla fupi
iliyofanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam
Akipokea
vifaa hivyo Mama Pinda ameishukuru Vodacom kwa kuunga mkono juhudi za
kuyawezesha mashindano hayo kufanyika vema chini ya uenyeji wa Tanzania
kupitia chama cha Netiboli nchini – CHANETA.
“Nawashukuru
sana Vodacom mmetupatia zaidi ya kile tulichowaomba, hii sasa ni wazi
timu yetu ya Taifa Queens itafanya vizuri na kuibuka mshindi wa
mashindano hayo makubwa kwa netiboli Afrika”Alisema Mama Pinda.
Kwa
upande wake Bw. Mwalim alimpongeza Mama Pinda kwa kuwa mstari wa mbele
kuhakikisha mashindano hayo yanafana chini ya ardhi ya Tanzania
“Kwa
kweli mama umefanya kazi kubwa na nzuri sana inayostahili kila aina ya
pongezi ya kuzunguka kila mahali kuhamasisha watanzania kuyachangia
mashindano haya na timu yetu ya taifa – Taifa Queens, hakika umeonesha
mfano mzuri na wa kuigwa kwamba Netiboli ikisimamiwa kidete kama
ulivyofanya nayo chati yake itakuwa juu”Alipongeza Bw. Mwalim.
Bw.
Mwalim aliongeza kusmea kuwa Vodacom siku zote inajivunia ushiriki wake
katika kukuza michezo nchini ikitambua kuwa michezo ni eneo muhimu la
kuwaunganisha watanzania na kuwapatia wakati wa furaha baada ya pirika
za hapa na pale
“Vodacom
tunajivunia rekodi yetu ya kuendeleza na kukuza michezo nchini leo
taifa zima linapongezana na kupena pole kufuatia mechi ya jana ya Simba
na Yanga hayo ni matunda ya Vodacom kuweka udhamini katika soka na leo
tunajivunia kuiwezesha Taifa Queens kushiriki mashindano ya
kimataifa”Alisema Bw. mwalim
Mwisho
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)