MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMKARIBISHA MAKAMU WA RAIS WA IRAN KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMKARIBISHA MAKAMU WA RAIS WA IRAN KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Makamu wa Rais wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, wakati alipowasili  Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam kwa mazungumzo leo Mei 30, 2012. Makamu wa Rais wa Iran  amewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akipokea zawadi kutoka kwa Makamu wa Rais wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, baada ya  kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo Mei 30,  2012, (kulia) ni Waziri wa Kazi wa Iran, Sheykhales Lam (kushoto) ni Mkarimaniwa Makamu wa  Rais wa Iran.Makamu wa Rais wa Iran amewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku  tatu.
Makamu wa Rais wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, akiweka saini katika kitabu cha  Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  (katikati) wakati alipofika Ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo leo Me 30, 2012. Kulia  ni Waziri wa Kazi wa Iran, Sheykhales Lam. Makamu wa Rais wa Iran amewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Makamu wa Rais wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, wakati alipofika Ofisini  kwake Ikulu Dar es Salaam leo, Mei 30, 2012 kwa ajili ya mazungumzo. Makamu wa Rais wa  Iran amewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, baada ya kumaliza  mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo Mei 30, 2012.  Makamu wa Rais wa Iran amewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Makamu wa Rais wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, wakiwa katika mazungumzo maalum,  katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro Dar es Salaam leo Mei 30, 2012. Makamu wa  Rais wa Iran amewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu.Picha na Muhidin  Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages