MWANDISHI MWANAMKE ASHINDA KUONJA LADHA BIA ZA TBL MWANZA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

demo-image

MWANDISHI MWANAMKE ASHINDA KUONJA LADHA BIA ZA TBL MWANZA

DSC05073
Mshindi wa tatu wa shindano la kuonja na kutambua ladha ya bia za Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ambalo liliwashirikisha baadhi waandishi wa habari  Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Chacha  (kulia) wa ITV na Redio One, akipokea zawadi yake kwa furaha kutoka kwa Meneja wa kiwanda cha bia, TBL, Mwanza, Richmond Robert mwishoni mwa wiki.
DSC05071
Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Business Times Ltd, Mwanza Jovin Mihambi akikabidhiwa zawadi ya ushindi wa pili na Meneja wa kiwanda cha bia (TBL ) Mwanza Richomnd Robert, katika shindano la kuonja na kutambua ladha ya bia.
DSC05064
 Emmanuel Chacha wa ITV/ Redio Oneakifanya vitu vyake kwenye shindano la kuonja bia na kutambua ladha ya aina ya bia
DSC050521
 Waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza, wakishindana kuonja na kutambua ladha ya bia mwishoni mwa wiki katika Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha Mwanza. Kutoka kulia ni  Emmanuel Chacha wa ITV/ Redio One , Hellen Kabambo wa gazeti la Changamoto.
DSC05033
Waandishi wa habari wakimsikiliza Afisa Ubora wa Bia( TBL ) Jeremiah Kmammbi kuhusu bia inavyohifadhiwa .Waandishi walitembelea kiwanda hicho cha bia mwanza kabla ya kushiriki shindano la kuonja bia na kutambua ladha ya aina ya bia.
DSC050741
Waandishi walioshinda shindano la kuonja na kutambua ladha ya bia wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa zawadi zao. Kutoka kushoto ni Meneja wa kiwanda cha Bia (TBL) Mwanza, Richomd Robert,, Jovin Mihambi wa Business Times, Jacquline Wanna wa gazeti la Kasi Mpya amnbaye alishika nafasi ya kwanza sawa na Henry Kavirondo , Emmanuel Chacha wa ITV na Redio One (katikatia), mshindi wa kwanza Henry Kavirondo wa Chanel Ten na  Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TBL, Editha Mushi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Pages