RAZA AIBUKA MSHINDI JIMBO LA UZINI ZANZIBAR - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

RAZA AIBUKA MSHINDI JIMBO LA UZINI ZANZIBAR

Mh. Mohammed Raza

Na Khadija Khamis –Zahira  Bilali –MAELEZO
Tume ya Uchaguzi Zanzibar imemtangaza rasmi Mohamed Raza Hassanali Mohamadali  kuwa Mwakilishi halali wa Jimbo la Uzini kwa kushinda  asilimia 91.1 sawa na kura 5377.

Matokeo hayo yametolewa na Afisa Msimamizi Uchaguzi wa Wilaya ya Kati Mussa Ali Juma huko katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kati Unguja. Alisema kuwa  zoezi la Uchaguzi  mdogo wa Jimbo la Uzini ulikwenda vizuri mpaka kufikia katua ya matokeo.Alisema kuwa  Vyama vilivyoshiriki katika zoezi hilo vilikuwa  jumla ya vyama   vitano ndivyo vilivyoweza kusimamisha wagombea wake navyo  ni AFP,CCM,CHADEMA .CUF na  TADEA .

Matokeo ya uchaguzi huwo ulikuwa kama ifuatavyo kwa upande wa CCM mgombea wake Mohamedraza alipata kura 5377, Rashid Yussuf Mchenga wa AFP alipata kura 08  Khamis Khatib Vuai wa TADEA alipata kura 14 Salma Hussein Zaral wa CUF amepata kura 223,na Ali Mbaruku Mshimba wa CHADEMA  alipata 281 .

Alieleza kuwa jumla ya wananchi waliondikishwa katika uchaguzi huo ni 8743 waliyojitokeza kupiga kura 5931  kura halali  5903na kura zilizoharibika 28 .Nae Mgombea wa CCM aliebukia kuwa mshindi wa uchaguzi huo  aliishukuru Tume ya Uchaguzi   kwa kuendesha zoezi hilo kwa ufanisi .

Pia aliwahidi  wananchi wake wa  jimbo hilo kuwa atawatumikia bila ya  kujali ubaguzi na itikadi za  kisiasa na kuwaletea maendeleo kwa vitendo kama ilani ya chama chake inavyoeleza .Zoezi hilo  la uchaguzi limefanyika kutokana na kufariki kwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini  Marehemu Mussa Khamis Silima .  

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages