Zambia
imechukua ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2012 baada ya
kuwafunga Ivory Coast kwa mikwaju ya penati 7-8.Mchezo huo ulimaliza
dakika 90 za kawaida, kabla ya kwenda muda wa ziada, na hadi katika
mikwaju ya penati. Awali nahodha wa Ivory Coast, Didier Drogba alikosa
penati ambayo ingeipa ushindi kabla ya kumalizika kwa dakika 90 za
kawaida. Ivory Coast wamekosa penati 2 kati ya walizopiga ambapo Kolo
Toure na Gervinho walikosa mikwaju hiyo.
Ivory
Coast wataendelea kusubiri kunyakua kombe hilo, licha ya kuwa na
wachezaji kadhaa wanaocheza Ulaya hasa katika Ligi Kuu ya England.
Tembo wa Ivory Coast walipoteza katika mchezo wa fainali mwaka 2006
dhidi ya Misri kwa mikwaju ya penati. Lakini kwa Chipolopolo, ambao
wamewahi kushika nafasi ya pili mara mbili, wamemaliza kwa ushindi kwa
kuhanikizwa na vifo vya wachezaji wenzao mwaka 1993, baada ya ndege
yao kuanguka karibu na uwanja ilipochezewa fainali mjini Libreville.
Mara
ya mwisho kwa timu hiyo kutoka Kusini mwa Afrika kufika fainali
ilikuwa mwaka 1994, mwaka mmoja tu baada ya wachezaji 18 wa nchi hiyo
kupata ajali ya ndege karibu na mji mkuu wa Gabon. Wakielekea katika
mchezo wa fainali, wachezaji hao wa sasa walisema wanahisi nguvu
kutokana na kukumbuka janga lililowapata wenzao. Kwa kushinda mchezo wa
fainali, wameonesha dhamira ya kuwashinda wapinzani wao ambao
walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kupata ushindi.
Source BBC.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)