Mwili wa Marehemu Esther Badi aagwa leo - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mwili wa Marehemu Esther Badi aagwa leo

Jeneza la mwili wa marehemu mama Esther Badi ambaye ni mama mzazi wa aliyekuwa katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Brandina Nyoni, na Mpigapicha wa Magazeti ya This Day na Kulikoni, John Badi likiwa  ibada maalum ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika leo kwenye kanisa kilutheri la Azani Front jijini Dar es salaam leo, mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda mkoani Iringa na utazikwa katika kijiji cha Ilembula huko Njombe. 
Bi. Blandina Nyoni Mtoto wa Marehemu mama Esther Badi akitoa historia ya marehemu wakati wa ibada hiyo leo.
Waombolezaji mbalimbali wakiwa katika ibada hiyo.
Ndugu na jamaa wakiwa katika ibada hiyo leo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dk. Hadji Mponda kulia akiwa pamoja na Paniel Lyimo katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu wamehudhuria ibada hiyo pia.

Mwili wa marehemu ukiandaliwa tayari kwa waombolezaji kuanza kutoa heshima zao za mwisho.
Paniel Lyimo katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (kulia)akitoa heshima zake za mwisho mbele ya jeneza la mwili wa marehemu Mama Esther Badi.
Waombolezaji wakielekea kutoa heshima zao za mwisho.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages