Mkuu
wa Wilaya ya Moshi Alhaji Mussa Samizi (kulia) akikabidhi zawadi ya
Simu, fedha Tsh 80,000 na Mordem iliyo na kifurushi cha kuanzia
20,000/= kwa mshindi wa pili wa mbio za Vodacom Fun Run, Brazil Boay
katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2012 zilizofanyika jana mjini
Moshi. Katikati ni Mkuu wa Udhamini wa Vodacom, George Rwehumbiza.
Mkuu
wa Wilaya ya Moshi Alhaji Mussa Samizi (kulia) akikabidhi zawadi ya
Simu, fedha Tsh 80,000 na Mordem iliyo na kifurushi cha kuanzia
20,000/= kwa mshindi wa tatu upande wa wanawake Natalia Elisante, wa
mbio za Vodacom Fun Run, Brazil Boay katika mashindano ya Kilimanjaro
Marathon 2012 zilizofanyika jana mjini Moshi. Katikati ni Mkuu wa
Udhamini wa Vodacom, George Rwehumbiza.
Mkuu
wa Wilaya ya Moshi Alhaji Mussa Samizi (kulia) akikabidhi zawadi ya
Simu, fedha Tsh 100,000 na Mordem iliyo na kifurushi cha kuanzia
20,000/= kwa mshindi wa kwanza upande wa wanawake Jackline Sakilu, wa
mbio za Vodacom Fun Run, Brazil Boay katika mashindano ya Kilimanjaro
Marathon 2012 zilizofanyika jana mjini Moshi. Katikati ni Mkuu wa
Udhamini wa Vodacom, George Rwehumbiza.
Ofisa
Masoko Mkuu na Mahusiano Wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba
akishiriki katika mbio za kujifurahisha za”Vodacom 5 KM fun run”
Mmoja wa washiriki walemavu alieshiriki katika mbio za kujifurahisha za “Vodacom 5 KM fun run”akimaliza mbio zake.
Baadhi ya washiriki wa mbio za kujifurahisha za”Vodacom 5 KM fun run”wakimaliza mbio zao nakujinyakulia zawadi mbalimbali.
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Rukia Mtingwa wa pili toka kushoto
akifurahia jambo na baadhi ya watoto wenye ugonjwa wa ukimwi mara
walipomaliza kushiriki katika mbio za kujifurahisha za “Vodacom 5 KM fun
run”
Baadhi
ya washindi wa Vodacom 5 KM fun run wakiwa kwenye picha ya pamoja na
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Rukia Mtingwa kulia na Afisa
Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude kushoto.
---
Mbio
za kujifurahisha za kilometa 5 za (Vodacom 5KM fun run) ambazo ni
sehemu ya mbio za Kilimanjaro marathoni zimezidi kujizolea umaarufu kwa
watu wengi wa rika tofauti kujitokeza kushiriki kwenye mbio hizo
zilizofanyika jana/leo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kwa
mujibu wa Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mahusiano wa kampuni ya
Mawasiliano ya Vodacom Tanzania ambao ndio wadhamini wa mbio hizo,
Rukia Mtingwa katika mbio za mwaka huu jumla ya watu 10,000
wamejitokeza kushiriki kwenye mbio hizo tofauti na makadirio ya
kawaida ya kupata jumla ya washiriki 5000 ambacho ndicho huwa kiwango
cha juu .
Mtingwa
alisema wengi wa washiriki katika mbio hizo kwa mwaka huu zimetokana
na uhamasishaji mkubwa uliofanywa na vyombo vya habari na mvuto wa mbio
hizo ambazo huambatana na manjonjo mbalimbali Kutoka kwa washiriki wake
na zawadi za kuvutia zinatolewa na Vodacom.
Pamoja
na mafanikio hayo Mtingwa alisema wao kama wadhamini wamepata
changamoto kubwa katika mbio hizo hasa kwa mwaka huu kutokana na
wakimbiaji wazoefu kujitosa kushiriki kwenye mbio hizo badala ya
kuwaachia watu wengine ambao riadha sio fani yao .
“Kwa
kweli mwaka huu tumekumbana na changamoto hiyo ya wakimbiaji profession
kushiriki kwenye fun run ambazo sisi tunaona ni maalum kwa watu ambao
riadhi si fani yao kwahiyo kipindi kijacho endapo tutaendelea na
udhamini wa mbio hizi itabidi tuifanyie kazi changamoto hii,”alisema
Mtingwa .
Aidha
Mtingwa alisema changamoto ya kujitokeza washiriki wengi kwao ni faraja
kubwa na watajipanga kukubaliana na haki hiyo ili kuendana na
mazingira ya ukubwa wa mbio hizo kadiri watu watakavyokuwa
wakijitokeza.
Washindi
wa mbio za jana/leo kwa upande wa wanaume ni Gailet Ismail ambaye
alichukua na nafasi ya kwanza na kujinyakulia simu ya mkononi aina ya
ZTE S- 501,muda wa maongezi wa Sh 20,000, modem ya intaneti pamoja na
M-Pesa ya Sh 100,000.
Brazil
Boay alichukua nafasi ya pili na kuzawadiwa simu ,muda wa
maongezi,modem ya intanert na M-Pesa ya Sh 80,000 wakati mshindi wa
tatu alikuwa Fabiano Nelson ambaye naye alipata simu,muda wa
maongezi,modem na M-Pesa ya Sh 60,000.
Na
upande wa wanawake washindi walikuwa ni Jackline Sakilu,Catherine
Iranga na Natalia Elisante ambao nao walijishindia zawadi sawa na zile
walizopata wanaume , washindi wengi kuanzia nafasi wanne hadi 10 pamoja
na wshiriki walioweza kumaliza mbio hizo nao walipata zawadi mbalimbali
kutoka Vodacom.
Huo
ni mwaka wa tano tokea Vodacom iwe mdhamini wa mbio za kilometa tano
za kujifurahisha (Vodacom fun run) ambazo ni sehemu ya mbio maarufu za
Kilimanjaro ambazo mwaka huu zimeadhimisha miaka 10 tokea kuanzishwa
kwake .
Mwisho.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)