Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwasili kwenye eneo la Soko la Tunduma jana, kwa ajili ya kuzindua
soko hilo baada ya kukamilika kwa ukarabati wake kufuatia moto
ulioteketeza soko hilo mwaka jana. Makamu wa Rais amewasili mkoani Mbeya
jana kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akikata utepe kuzindua Soko la Tunduma lililofanyiwa ukarabati baada ya
kuungua moto mwaka jana, wakati akianza rasmi ziara yake ya kikazi
katika Mkoa wa Mbeya jana. Kushoto ni Mkewe Mama Asha Bilal, (kulia) ni
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na (kulia kwake) ni Mbunge wa Mbozi Magharibi David Silinde.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwahutubia wananchi wa Tunduma wakati alipofika eneo hilo kwa ajili
ya kuzindua Soko la Tunduma baada ya kukamilika kwa ukarabati kufuatia
soko hilo kuungua motoa mwaka jana.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)