MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AMALIZA ZIARA YAKE YA MKOA WA RUKWA NA KATAVI KWA KUZINDUA KAMPENI YA SUMBAWANGA NG’ARA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AMALIZA ZIARA YAKE YA MKOA WA RUKWA NA KATAVI KWA KUZINDUA KAMPENI YA SUMBAWANGA NG’ARA

 Makamu wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Kampeni ya Sumbawanga Ng’ara yenye lengo la kudumisha usafi wa mazingira mjini Sumbawanga, wakati akimalizia ziara yake ya mkoa wa Katavi na Rukwa jana. Kulia kwake ni mkewe Mama Asha Bilal na kushoto kwake ni Mkuu wa  Mkoa wa Katavi na Rukwa, Eng. Stella Manyanya.
 Mama Asha Bilal, akionyesha mfano kwa kufagia wakati akimkabidhi mmoja wa kinamama wanaofanya usafi wa mazingira katika mitaa ya mjini Sumbawanga, jana wakati Makamu wa Rais alipokuwa akizindua kampeni ya Sumbawanga Ng’ara yenye lengo la kudumisha usafi wa mazingira.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa viongozi wa kampuni za kufanya usafi katika mitaa ya mjini Sumbawanga, wakati akizindua kampeni ya Sumbawanga Ng’ara  kwa ajili ya kudumisha usafi wa mazingira, ikiwa ni siku yake ya mwisho ya ziara yake katika mkoa wa Katavi na Rukwa jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mama Asha Bilal (kushoto kwake) na Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Rukwa, Eng. Stella Manyanya (kulia kwake) na baadhi ya viongozi wa mji wa Sumbawanga, mbele ya Sanamu la Sumbawanga Ng’ara baada ya kuzindua kampeni hiyo jana.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages