Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo na kutazama mmoja kati ya mizinga ya Nyuki kutoka
kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, kuhusu utengenezaji wa Mizinga
hiyo ya kisasa na gharama nafuu, wakati alipofika kutembelea kituo cha
kuahiria mifugo cha Simambwe, kilichopo Wilaya ya Mbeya Vijijini, akiwa
katika ziara yake ya mkoa wa Mbeya jana Februari 25, 2012. Kulia ni Mke
wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilal.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi mzinga wa Nyuki mmoja kati ya wafugaji , Salome Zumba wa
Kikundi cha kinamama na Vijana cha kijiji cha Ijewe, wakati alipokuwa
katika ziara yake ya mkoa wa Mbeya jana Februari 25, 2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akinyoosha mkono kuwasalimia wananchi wa Kijiji cha Simambwe, wakati
alipowasili kijijini hapo kutembelea Kituo cha Kuahiria Mifugo na
kukabidhi mizinga ya nyuki kwa badhi ya wafugaji, akiwa katika ziara
yake mkoa wa Mbeya jana Februari 25, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)