Musa baada ya matibabu anavyoonekana sasa
Musa kabla ya kumwagiwa tindikali
MKAZI
wa Igunga mkoani Tabora, Mussa Tesha (24) aliyekuwa akipata matibabu
India baada ya kuwagia tindikali na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa
Chadema wakati wa kampeni za uchagfuzi mdogo jimboni humo Septemba mwaka
jana, amerejea nchini.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba
alisema leo kwamba, Tesha amerejea akiwa amepona kiasi cha kuweza
kuzungumza na kuona jicho moja huku lingine likiwa bado halioni vizuri
kutokana na athari alkizopata.
Akizungumza
nyumbani kwake Tegeta Mwisho, Dar es Salaam, Mwigulu ambaye alikuwa
Meneja wa Kampeni za CCM Igunga, alisema amemhifadhi Tesha nyumbani
kwake wakati akisubiri kwenda tena India kuendelea kuendelea na matibabu
madogo yaliyosalia.
Mwigulu
alisema, Chama Cha Mapinduzi ambacho kiligharamia matibabu yote, hadi
sasa kinaendelea kumhudumia Tesha mpaka atakapopona kabisa na kuwa na
uwezo wa kufanya kazi.
"Hadi
sasa tunashukuru kwamba amepona anaweza kuzungumza, kusikia na kuona
walau jicho moja, tofauti na mwanzo alivyokuwa mara alipomwagiwa
tindikali, hata hivyo hali yake haijaweza kuwa ya kufanya kazi
mbalimbali kama za juani, hivyo CCM tunaendelea kumsaidia mpaka ajenge
uwezo wa kujitegemea", alisema.
Alisema,
CCM imefanya mpango wa kuwaugnanisha wabunge wa CCM kumtayarishia mtaji
ambao utamsaidia Tesha kuendesha maisha yake baada ya kukumbwa na
madhara hayo.
Akizungumza
kwa mara ya kwanza tangu amwagiwe tindikali, Tesha amewashukuru
Watanzania kwa kumuombea wakati wote alipokuwa mgonjwa na kwamba
anaamini dua zao ndizo zimemwezesha kubakia hai hadi sasa.
Tesha
alisema, baada ya kumwagiwa tindikali Septemba 9, mwaka jana,
hakujitambua hadi alipokuwa katika hospitali ya KCMC ambako alipatiwa
matibabu na baadaye kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alikaa
wiki tatu kabla ya kupelekwa India.
Akiwa
India kwenye Hospitali ya Apollo, Tesha alikuwa chini ya uangalizi wa
baba yake mdogo, Samwel Bethwel ambaye pia gharama za kuwa huko
zimebebwa na CCM. Anatarajia kwenda tena India baada ya miezi mitatu.
Na Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)