Chama
Cha Mapinduzi kimepokea kwa majonzi makubwa taarifa za kifo cha Mbunge
wa Viti Maalum kupitia Chadema Marehemu REGIA MTEMA kilichotokea leo kwa
ajali ya gari katika wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Chama
Cha Mapinduzi kinatoa salamu za pole kwa CHADEMA, familia ya marehemu,
ndugu, jamaa na marafiki pamojan na watanzania wote kwa ujumla.
Marehemu
MTEMA amekuwa na mchango mkubwa kwa wananchi wa kada zote wakiwemo watu
wenye ulemavu ambao kwa sehemu kubwa alikuwa akiwatetea na kuwasemea
katika mijadala mbalimbali ndani na nje ya Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Alikuwa
ni Kiongozi aliyetetea na kuusimamia Utaifa hata pale masuala ya
kiitikadi yalipokuwa yakitaka kuchukua nafasi kubwa, jambo ambalo
lilisukumwa na kiwango cha uzalendo alichokuwa nacho.
Chama
Cha Mapinduzi kinaungana na watanzania wote kuomboleza msiba huu
mkubwa, kwa familia yake, Chadema, siasa ya Tanzania na kwa Bunge la
Jamhuri ya Muungano ambakoi ndiko alikokuwa akitumikia jukumu la
uwakilishi wa wananchi.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe.
Nape M. Nnauye
Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa
Itikadi na Uenezi
Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM
14-01-2012
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)