Meneja
wa Tigo kwa mikoa ya Dodoma na Singida Fadhila Saidi akimuonyesha mmoja
wa wanafunzi wa Chekeckechea katika shule ya Msingi ya Kizota ya mjini
Dodoma jinsi ya kutumia vibao vya kujifunzia. Jumla ya vibao 1000
vilikabidhiwa shuleni hapo na kampuni ya Tigo.
Meneja
wa Tigo kwa mikoa ya Dodoma na Singida
Fadhila Saidi (katikati) akimkabidhi vibao vya kujifunzia mwalimu mkuu
wa shule ya msingi ya Kizota ya mjini Dodoma , Mwalimu Juma Malecela
(kushoto). Tigo ilikabidhi vibao 1000 katika shule hiyo. Kulia ni Dotto
Mwantengwe mratibu wa elimu Kata ya Kizota
Walimu
wa shule ya msingi Kizota ya Dodoma Olimpia Mbuga na Felician Rocky
wakiwalekeza wanafunzi jinsi ya kutumia vibao vya kujifunzia
vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo. Tigo ilikabidhi
jumla ya vibao 1000 katika shule hiyo
= = = = = = = = = = = =
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tigo yasaidia shule Dodoma
September 12, 2011, Dodoma,
Katika jitihada zake za kusaidia sekta ya elimu nchini Tanzania , kampuni ya simu za mkononi ya
Tigo imetoa msaada wa vibao vya kujifunzia 1000 kwa shule ya Msingi ya
Kizota ya mjini Dodoma .
Vibao hivyo vimetengenezwa kwa kutumia
plastik ili viweze kubebeka kwa urahisi. Juu ya vibao hivyo kuna michoro
na maandishi ya vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kumsaidia mwanafunzi
kujifunza. Kuna michoro ya maumbo mbalimbali kama
vile alfabeti, tebo ya kuzidisha na aina mbalimbali za rangi.
Kampuni ya Tigo imefikia umamuzi wa
kutoa msaada huo kwa kuthamini umuhimu wa elimu ya shule ya msingi hapa
nchini. Halikadhalika kwa kuzingatia kuwa watoto wa leo ndiyo watakuwa
viongozi wa kesho kwahiyo ni vyema kuwaboreshea mazingira ya elimu.
Mwakilishi wa Tigo Fadhila Saidi ambaye
ni meneja mauzo wa mikoa ya Dodoma na Singida alisema kuwa “Tunajisikia
furaha sana kuwasaidia watoto hawa ambao ni viongozi wa kesho ili
kuwarahishia njia ya kuzidi kujifunza hata kwa muda wao wa ziada na
kuongezea kuwa wanafunzi anaweza kutumia vibao hivyo kujifunza vitu
mbalimbali kwa wakati wake baada ya muda wa masomo.
Alisema kuwa lengo la kutoa msaada huo
hasa ni kusaidia badhi ya shule za msingi hapa nchini ambazo zimekuwa
zikihitaji za nyenzo za kujifunzia na kuongezea kuwa msaada huo
utaendelea kutolewa katika shule nyingine za msingi hapa nchini.
“Lengo letu ni kusaidia sekta ya elimu
hapa nchini na baada ya mradi huu kuna kitu kingine ambacho sisi kam
Tigo tunatarajia kukifanya hivi karibuni kwa ajili ya kusaidia tena
elimu hapa nchini,” alisema Fadhila.
Hivi karibuni kampuni ya Tigo
iliendesha kampeni maalum ya Tigo Tuchange yenye lengo la kuchangia
sekta ya elimu hapa nchini. Kiasi cha pesa kilichopatikana kitatumika
kununua vitabu kwa jili ya kusaidia baadhi ya shule za msingi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)