Ifahamu teknolojia ya Blind Spot kwenye Magari ya Kisasa - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Ifahamu teknolojia ya Blind Spot kwenye Magari ya Kisasa


Kadri siku zinavyosonga mbele kwa kasi ndivyo na teknolojia inakua kwa kasi ya ajabu sana huku watengenezaji wa magari nao wakienda sambamba na teknolojia. Leo tutaangazia teknolojia ambayo sio mpya sana lakini inapatikana katika magari mengi ya kisasa ambayo ni teknolojia mojawapo ya usalama katika gari pindi dereva anapoendesha gari. Teknolojia hii inaitwa BLIND SPOT MONITORING

Hatutarajii dereva kuwa na macho nyuma ya kichwa chake hivyo kumfanya ashindwe kufahamu yanayoendelea nyuma bila msaada wa kuwa na vioo vya kumuonyesha nyuma yaani kioo cha kushoto, kulia na nyuma (side mirrors and rear mirror) Basi kabla ya teknolojia hii ajali zilikuwa nyingi sana mdipo watengenezaji wa magari wakaona sasa katika kupunguza ajali waje na hii teknolojia. 

Hii teknolojia humsaidia dereva kufahamu yanayoendelea pande zote za gari yake ambazo hawezi kuona kupitia kioo chake cha mbele (Windscreen) ndipo hapo hii Blind spot humsaidia kufahamu nini kinaendelea katika upande ambao yeye hawezi kuona kupitia kioo cha mbele.

Teknolojia hii inafanyaje kazi?

Teknolojia hii inafanya kazi kupitia sensor mbalimbali zilizowekwa kwenye gari husika, sensa hizi husaidia kutoa taarifa ya nini kinaendelea pande zote za gari husika. Pindi sensa hizi zinapotoa taarifa kuwa kuna gari inakaribia gari lako au kuna kitu kina karibia kuingia kwenye eneo ambalo dereva hawezi kuona basi sensa hizo hutoa hutuma taarifa kwa haraka na hatimaye taa za upande husika kuwaka na kumuonyesha dereva huyo ndani kupitia dashbodi yake, na taa hiyo itaendelea kuwaka mpaka dereva wa gari husika atakapohama upande mwingine wa barabara au kuondoka katika eneo hilo 

Magari mengi ya kisasa yanakuja yakiwa na teknolojia hii ya usalama ambapo kuna baadhi ya magari kama Chevrolet Cruze na Mazda3 inabidi ununue na ufungiwe kwenye gari yako.

Teknolojia hii husaidia nini?

Teknolojia hii husaidia kupunguza au kuzuia ajali ya kugongana, kugongwa nyuma au kumgonga mtu au gari ambalo dereva hukuliona kupitia kioo chako cha mbele. Endapo dereva wa gari lenye hii teknolojia ataweza kufahamu kuwa kuna gari jingine au kizuizi katika eneo ambalo dereva huyo hawezi kuona kupitia kioo cha mbele au cha nyuma.

Tunaamini utaendelea kujifunza zaidi na zaidi

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages