NMB WADHAMINI MASHINDANO YA GOLF YA MKUU WA MAJESHI, JWTZ - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NMB WADHAMINI MASHINDANO YA GOLF YA MKUU WA MAJESHI, JWTZ

Golf%2B1
Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB, Omari Mtiga (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya Shilingi milioni 26 Mwenyekiti wa klabu ya gofu Lugalo Brigedia Jenerali mstaafu, Michael Luwongo (katikati) zilizotolewa na NMB kudhamini Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi nchini yanayotarajia kufanyika Oktoba 13 katika viwanja vya Lugalo Dar es Saalam.

Golf%2B2
Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB, Omari Mtiga (kushoto) akimkabidhi moja ya jezi Mwenyekiti wa klabu ya gofu Lugalo Brigedia Jenerali mstaafu, Michael Luwongo zilizotolewa na NMB ikiwa ni sehemu ya udhamini wa Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi nchini yanayotarajia kufanyika Oktoba 13 katika viwanja vya Lugalo Dar es Saalam.

BENKI ya NMB imedhamini Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi nchini yanayotarajia kufanyika Oktoba 13 na kushirikisha wachezaji wa gofu kutoka klabu mbalimbali nchini.

Udhamini uliotolewa ni wa shilingi milioni 26 pamoja na vifaa mbalimbali zikiwemo jezi zitakazo tumika katika mashindano hayo vimekabidhiwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB, Omari Mtiga katika viwanja vya Lugalo.

Kukabidhiwa kwa udhamini huo ni mwendelezo wa Benki ya NMB kudhamini na kusaidia shughuli anuai za michezo hususani ya Jeshi la wananchi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kukabidhiwa kwa udhamini huo, Makamu Rais wa Umoja wa Klabu za Golf Tanzania, Luteni Canali David Luoga alisema mashindano hayo yanatarajia kushirikisha wachezaji kutoka vilabu mbalimbali vya golf Tanzania na makundi ya wachezaji wakiwemo watoto.

Alisema mashindano hayo ambayo yatafanyika kwa siku moja pekee na kufunguliwa na Mkuu wa Majeshi  ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo washindi watajipatia fedha taslimu pamoja na vikombe.

Aliongeza kuwa mashindano hayo yatakuwa na mvuto wa pekee kwa kile kushirikisha viongozi waandamizi mbalimbali kutoka Serikalini waliostaafu na awaliopo madarakani.


No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages