Pages

MAFANIKIO TUNAYOYAPATA NI MABORESHO NA MAONI YA WATEJA - NMB

DSC_1027
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya NMB, Omari Mtiga pamoja na baadhi ya wateja Benki ya NMB waliojumuika kwenye hafla ndogo ya kuwasikiliza wateja katika tawi hilo wakikata keki maalum ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

DSC_1052
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya NMB, Omari Mtiga akimkabidhi cheti maalum Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Chasco Traders, Sando Chasco ambaye ni mteja aliyetukuka wa Benki ya NMB kwa muda mrefu sasa. Mteja huyo amepata mafanikio katika biashara yake baada ya kukuwa na huduma za kibenki za NMB, alianza kukopa shilingi 300,000 na sasa anapata mkopo wa zaidi ya milioni 100 kuendesha biashara zake. 

DSC_1028
Meneja wa NMB Tawi la Ilala jijini Dar es Salaam, Kidawa Masoud akiandaa keki maalum ya wateja kabla ya kuanza kuwalisha wateja wa NMB Tawi la Ilala walioshiriki katika hafla hiyo.

DSC_1030
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya NMB, Omari Mtiga akimlisha keki Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Chasco Traders, Sando Chasco (kulia) ambaye ni mteja aliyetukuka wa Benki ya NMB kwa muda mrefu sasa.

DSC_1031
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya NMB, Omari Mtiga (kulia) akimlisha keki mmoja wa wateja wa NMB Tawi la Ilala walioshiriki katika hafla hiyo.

DSC_1036
Meneja wa NMB Tawi la Ilala jijini Dar es Salaam, Kidawa Masoud akiwalisha keki baadhi ya wateja wa NMB Tawi la Ilala walioshiriki katika hafla hiyo.



BENKI ya NMB imesema maboresho makubwa iliyoyafanya ni matokeo ya mirejesho kutoka kwa wateja wake. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB, Bw. Omari Mtiga alipokuwa akizungumza na Baadhi ya wateja wa Benki hiyo Tawi la Ilala ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja.

"...Maboresho makubwa tuliyoyafanya ni matokeo ya mirejesho kutoka kwa wateja wetu ambayo tumeyapokea siku za nyuma. Siku zote tunatambua na kushukuru kwa michango na maoni ya wateja wetu, ndio sababu ya kuendelea kuwa nao bega kwa bega," alisema Bw. Mtiga.
Aliongeza kuwa NMB inatambua ushindani mkubwa uliopo na itaendelea kukabiliana nao kwa kadri unavyo kua siku hadi siku. Alisema kwao ushindani wanaupenda na wanachukulia kama fursa ya kufanya vizuri zaidi. "...Ushindani ni fursa nzuri maana inatufanya kubuni bidhaa bora kulingana na mahitaji ya wateja na kufanya vizuri zaidi kwa wateja wetu."

Alisema wiki ya huduma kwa wateja tangu ilipoanza NMB imepata fursa ya kujumuika na wateja wake maeneo mbalimbali na kupata mrejesho kwa masuala mbalimbali juu ya huduma zao na ndio maana inachukulia uzito mkubwa kuzungumza na wateja na kutupa mrejesho ili kuweza kuifanyia kazi.

"...Sisi kwetu tunaiona kama fursa ya pekee kukutana na wateja na kupata maoni yao lengo likiwa ni kuboresha zaidi huduma zetu. Lakini tumekuwa tukifarijika zaidi kwani mbali na mrejesho kuna maeneo ambayo wametutia moyo kwamba tunafanya vizuri hivyo tunawaahidi kuongeza juhudi ili kusonga mbele zaidi."

Tunasema hatubweteki kwa pongezi kwani ushindani ni mkubwa nasi tuna ahidi kufanya vizuri zaidi ili kumfanya mteja afurahiye huduma zetu. Tutaendelea kuboresha na kuangalia mteja wetu anataka nini "Sisi kama taasisi tunasema kwamba tumejipanga na tuko vizuri, tunajiamini na huduma zetu kwa namna tunavyoziboresha.

"...Tunacho waahidi wateja kwa sasa ni kwamba mbali na maboresho tunayoyafanya tutaendelea kukutana nao pia kuchukua mrejesho kutoka kwao...haturidhiki na kudhani tulipofika ni hatua ya mwisho bali tunaendelea kupokea mrejesho siku zote na tunaifanyia kazi hivyo wateja wetu waendelee kutushauri kwani maoni yao ni muhimu kwetu. Tutaendelea kuwapa huduma zile wanazopenda na hata nzuri zaidi ya wanavyoamini, ushahidi wa kufanya hivyo tunao maana mambo mengi wanaotushauri tumeyafanyia kazi kwa maboresho makubwa,"

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Chasco Traders, Sando Chasco ambaye NMB imemtunuki cheti maalum kwa kuwa mteja wa mfano, alisema NMB imemtoa mbali tangu miaka ya nyuma alipoanza na mtaji wa mkopo wa chini kama lakini tatu lakini sasa anaongelea kupata zaidi ya miliomi 100 jambo ambalo anaona ni mafanikio makubwa.

"Kiujumla binafsi NMB ni benki ambayo imenisaidia sana kwani nafanya biashara hadi mikoani na matawi wa benki hiyo yapo kila mahali hivyo inanisaidia kutotembea na mzigo wa fedha hasa dunia ya leo ambapo ni hatari kutembea na fedha. Nafanya mihamala yangu yote ya kuwalipa na kulipwa na wadeni wangu kupitia benki ya NMB. Nimekuwa pia ni balozi mzuri kila ninapofanya biashara zangu kuwashauri kuitumia benki hii kwa usalama wa shughuli zao." alisisitiza mteja huo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)