Pages

Tumsaidie Tuwezavyo - Anahitaji Msaada wa Haraka Ili tu Kuokoa Maisha Yake

Naitwa MISHALY SUMARY naishi Kibaha Maili moja, nilikuwa nikifanya kazi katika Hospitali ya Burere kama Muuguzi kuanzia mwaka 2008 mpaka tarehe 26/12/2011 siku ambayo sitaweza kuisahau katika historia ya maisha yangu, nilikuwa natoka kazini naenda nyumbani majira ya SAA 12 jioni nikiwa Njia ghafla nilivamiwa Na watu nisiyo wafahamu walikuwa wanaume wawili waliotokea nyuma yangu, mmoja alinishika shingoni na mwingine alinishika miguuni yule aliyenishika shingoni aliniambia sali dua yako ya mwisho Leo ni mwisho Wa maisha yako.
Walinipiga sana na wakanivunja uti Wa mgongo, nyonga, taya, meno Na shingo, nilipata maumivu makali Sana nililia kwa uchungu huku nikipiga kelele za kuomba msaada, kwa mbali zilisikika sauti za watu wakisogelea eneo lile mmoja kati ya wale wanaume wale wasiyo Na uruma alisema tumalize kazi tunauza gazeti, walichukua chuma na kunipiga usoni maeneo ya mdomo na kunivunja taya Na meno, wasamaria wema walipofika watu wale wasiyo Na huruma walikimbia Na kuingia vichakani, nipelekwa kituo cha polisi kupata PF3 nakupelekwa hospital ya Tumbi hali yangu iliendelea kuwa mbaya ambapo nilipata Rufaa ya kwenda Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kwa bahati mbaya nilikutana Na mgomo mkali Wa madaktari Na hali iliendelea kuwa mbaya Sana kwani viungo vyangu viliendelea kuingia ganzi mwishowe nikapoteza fahamu. Nilirudishwa katika Hospitali ya Burere ambako nilikuwa nafanyia kazi na kupatiwa vipimo ambavyo vilionesha kuwa pingili 3 za uti mgongo Na shingo ilikuwa zimepanguka, nililazwa pale kwa muda wa miezi 8 nikarudishwa MOI kwa madaktari bingwa Wa mishipa ya fahamu, waliniambia kwamba wangenifanyia operation ya Uti Wa mgongo ila kulikuwa Na uhaba Wa vitanda.
Niliendelea kuhudhuria kila tarehe nilizopangiwa, mwisho waliniambia hawawezi kunifanyia operation kwani maisha yangu yatakuwa hatarini, kiukweli niliumia Sana kupokea majibu hayo... Walinipa rufaa tena kwenda Daktari bingwa wa Mishipa ya fahamu kwani yeye ndiye angetoa maamuzi nifanyiwe operation au nisifanyiwe, nilipipelekwa kwa Daktari bingea huyo alisema operation hii ni ngumu inachukuwa zaidi ya SAA 8 hivyo Kama kuna uwezekano nipelekwe India, lakini wakati nikisubiri kwenda India nilitakiwa kuchongeshewa Viatu kwani miguu ilikuwa ikitoa Maji, kunywea Na kupinda, pia nilitakiwa kufanya mazoezi kila siku Na kumeza Dawa ya kulisha never zisiendelee kunywea.
Nilirudisha Muhimbili kwa mazoezi Na kuchongeshewa Viatu, nikiwa kliniki dada mmoja alinisogelea na kunijulia hali baada ya kuzungumza na kumuelezea hali halisi aliniahidi atakuja kuniona nyumbani , kweli siku chache baadaye alinitembelea nyumbani nakujitambulisha kuwa yeye ni Mwandishi Wa habari, nilimwelezea hatua ambayo tayari nilikuwa nimeshafikia kuwa nimeshatuma vipimo nje ya nchi (India) ila sina pesa Na family pia haina uwezo.. Aliniambia atairusha habari kwenye gazeti nitapata msaada Wa kwenda kutibiwa kweli namshukuru Mungu kupitia habari hile ilinikutanisha Na Baba mmoja Wa kule nyumbani Arusha yeye aliniambia anastaafu Kama nitakuwa sijapata pesa ya matibabu atanisaidia napia atawaomba marafiki zake wamsapoti.
Yule baba Alituma vipimo India walimjibu kuwa wanaweza kunitibu mgongo pekee kwa $ 18,000 na nitatakiwa kukaa kule kwa siku 18. Nilifanikiwa kwenda India kwa udhamini wa huyo baba lakini nilipofika hospitalini India walifanya vipimo upya wakagundua shida ni kubwa siyo sawa na vipimo vya Tanzania vilivyo kuwa vimetumwa mwanzo, hivyo Nikaambiwa kuwa natakiwa kukaa miezi 6 badala ya siku 18 kama ilivyokuwa mwanzo kabla ya kuondoka nchini, gharama ziliongezeka.
Nikiwa India waligundua nerves zote zilikuwa zimesinyaa na haziwezi kufanya kazi kabisa yaani nilikuwa nimepooza mwili mzima, kwahiyo wakaanza ku bust zile nerves kwanza maana Zilikuwa 0 zikapanda mpaka 46 . Na baadhi ya viungo kama mikono vikaanza kufanya kazi na nikawa na uwezo wa hata kujiburuza mwenyewe na kuketi.... Kwahiyo matumaini ya kupona yakaanza kurejea. Lakini baada ya miezi 3 ile pesa niliyokwenda nayo ikaisha kabisa na hakuwa na namna tena na mdhamini akawa hana njia nyingine ya kunisaidia.
Nilirejea Tanzania kutafuta namna ya kupata pesa ili nikamalizie matibabu lakini sikuweza kufanikiwa mpaka sasa ninavyoandika ujumbe huu...
Kwa sasa viungo vyote vimeanza kurudi katika hali ya mwanzoni kabla ya kwenda India. ile ganzi tena imerudi mwilini na mkono mmoja tu sasa ndo unaweza ku move. Ninaomba msaada kwa watanzania wenzangu ili niweze kupata pesa kwa ajili ya matibabu ambapo kwa makadirio si chini ya $ 20,000/- sawa na 40m.
Naomba kwa yeyote anayeweza kuniunganisha na Taasisi au mtu mwenye uwezo wa kunisaidia anisaidie. *Namba zangu ni 0718 797 494*
*MWENYEZI MUNGU AWABARIKI*

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)