Pages

Airtel, Benki ya Letshego na Jumo waungana ili kuwezesha wateja wao kuweka akiba kupitia Timiza Akiba.

 Mkurugenzi wa Biashara Airtel Tanzania Rohit Tandon akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa TIMIZA AKIBA ambayo ni huduma itakayowezesha wateja wa Airtel Money kujiwekea Akiba wao wenyewe kwa kutumia simu zao za mkononi wakiwa mahali popote. Huduma ya TIMIZA AKIBA ni ushirikiano baina ya Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money, Benki ya Letshego na watoa huduma ya teknolojia JUMO Tanzania.
 Mkurugenzi wa Biashara Airtel Tanzania Rohit Tandon wa kwanza kushoto, Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Benki Kuu ya Tanzania James Masoy wa pili kulia, Mkurugenzi wa biashara JUMO Tanzania Townsend Rose wa kwanza kulia na Mwenyekiti wa Bodi wa Benki Letshego Tanzania Simon Jengo kwa pamoja wakionyesha bango baada ya kuzindua TIMIZA AKIBA ambayo ni huduma itakayowezesha wateja wa Airtel Money kujiwekea Akiba wao wenyewe kwa kutumia simu zao za mkononi wakiwa mahali popote. Huduma ya TIMIZA AKIBA ni ushirikiano baina ya Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money, Benki ya Letshego na watoa huduma ya teknolojia JUMO Tanzania.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Benki Kuu ya Tanzania James Masoy akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa TIMIZA AKIBA ambayo ni huduma itakayowezesha wateja wa Airtel Money kujiwekea Akiba wao wenyewe kwa kutumia simu zao za mkononi wakiwa mahali popote. Huduma ya TIMIZA AKIBA ni ushirikiano baina ya Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money, Benki ya Letshego na watoa huduma ya teknolojia JUMO Tanzania.

  • Airtel Money, Benki ya Letshego na Jumo wazindua huduma maalum kwa wateja wao kuweka akiba kupitia Timiza
  • Akiba. Airtel, Benki ya Letshego na Jumo wawajengea wateja wao utamaduni wa kuweka akiba kupitia Airtel Money

Dar Es Salaam 30 Agosti 2018: Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money, Benki ya Letshego na watoa huduma ya teknolojia JUMO Tanzania wamefanya ushirika wa pamoja na kuzindua huduma kabambe itakayowawezesha wateja wao kuweza kujiwekea akiba wao wenyewe kwa kutumia simu zao za mkononi wakiwa mahali popote. TIMIZA Akiba ni huduma rahisi, isiyo na makato na itakayompa mteja zawadi ya fedha kila mwezi kwa kujiwekea akiba binafsi ili kufikia malengo. Zawadi hii itakuwa ni kiasi cha asilimia 5% ya salio l mteja aliloweka kama akiba ili kuhamasisha ari na ukuaji wa akiba.



Huduma hiyo maalum itakayojulikana kama TIMIZA AKIBA imezinduliwa leo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania wakati wa hafla maalum iliyofanyika katika ofisi za Airtel Makao Makuu. Huduma ya Timiza Akiba itakuwa suluhisho kwa wateja kuweza kuweka akiba kupitia simu zao za mkononi ambapo kwa sasa inapatikana kwa wateja wote wa Airtel Money. Wateja wa Airtel Money wataweza kujiwekea akiba zao bure kabisa kuanzia kiwango cha chini kabisa cha TSH100 na watakuwa wanapata riba kila mwezi. Huduma ya TIMIZA Akiba inatumia mfumo usiotoza ada wala gharama za uendeshaji kwani baada ya mteja kupata gawio la faida yake ya akiba ya kila mwezi mteja ataendelea kubaki na kiasi kilekile alichojiwekezea. Mfumo huu wa uendeshaji wa  huduma hii ya Timiza Akiba unadhamiria kukamilisha lengo la  ushirikiano kati ya Airtel, Benki ya Letshego  na JUMO la kuendelea kutumia teknolojia na kubuni huduma bora zaidi ili kuongeza kasi ya utoaji wa huduma jumuishi za kifedha kwa Watanzania.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutambulisha huduma ya TIMIZA AKIBA, Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Benki Kuu ya BoT James Masoy alisema ni faraja sana benki ya biashara, kampuni ya simu pamoja na kampuni ya mikopo midogo midogo kukaa pamoja na kushirikiana kufikisha huduma za fedha kwa wananchi. ‘Mmeamua kuweka ushindani wa kibiashara pembeni na kujumuika pamoja kuhudumia wananchi katika kuunga mkono Mpango wa Serikali wa Huduma za Kifedha Shirikishi’, alisema Majoy.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso, alisema “Airtel Tuna furaha kwa kuendelea kuwahudumia zaidi wateja wetu kupitia TIMIZA Akiba, tunaamini huduma hii itawawezesha kujiwekea akiba zao kwa uhakika zaidi. Tumedhamiria kuendeleza ubunifu kila siku ili   kurahisisha huduma za kifedha hapa nchini ziendelee kuwa rahisi na   kuwanufaisha watu wengi pale wanapozitumia. Tunataka huduma zetu ziwe sambamba na  mahitaji yao na ziwe suluhisho la mipango ya wateja wetu ya baadae”

“Wateja watakaoamua kutenga na kuweka kiasi kidogo cha fedha zao kama akiba badala ya kutumia fedha zote watapata zawadi.  Tukijua Kabisa kwamba leo hii watu wengi hawana utamaduni wa kujiwekea akiba, TIMIZA Akiba inatupa Watanzania fursa ya kujiwekea akiba ambayo itatusaidia kukabiliana na dharura na majanga yasiyotarajiwa kwa siku za baade”. Alielezea Colaso

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Letshego Bank Tanzania, Thabit Ndilahomba, amesema, “Timiza Akiba ni matokeo ya ushirikiano wa kweli unaolenga  kuboresha maisha ya wateja kama ilivyo ahadi yetu ambayo ni (Lets Improve Lives).  Ushirikiano  unabaki kuwa nyenzo yetu muhimu katika nchi zote 11 tunazoendesha shughuli zetu Afrika ikiwemo Tanzania.  Tukiwa  pamoja na Airtel na JUMO, tunatarajia kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba na kuongeza manufaa ya  kuweka akiba kwa Watanzania wote, popote walipo.” 

Nae Mkurugenzi wa Huduma wa JUMO Tanzania James Townsend-Rose, amesema, “Malengo yetu kama JUMO ni kuhakikisha tunatoa  zaidi huduma  mahsusi na madhubuti za fedha kwa watu ambao wakati mwingine ilikuwa ni vigumu kwao kupata huduma rasmi za fedha. Timiza Akiba ni mfano mmoja tu wa kile tulichoweza kufanikiwa kukifikia wakati tunajiandaa kuwapa thamani halisi wateja wetu kwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za fedha.”

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)