Pages

NMB YATOA MAFUNZO KWA ZAIDI YA VYAMA VYA MSINGI 1, 000 VYA USHIRIKA

1%2B%25289%2529
Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania - Benjamin Mkapa akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa NMB Bank – Ineke Bussemaker ikiwa ni shukrani kwa udhamini wa Maonesho ya Nane Nane Kitaifa yaliyofanyika atika viwanja vya Nyakabindi, Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu. NMB ilikuwa mmoja wa wadhamini wakuu wa maonesho hayo. 

3%2B%25285%2529
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu,Jenesta Mhagama(kulia) akiwakabidhi Meneja Uhusiano Biashara za serikali wa benki ya NMB,Christabel Hiza(kushoto) na Meneja Uhusiano Mwandamizi idara ya Kilimo biashara,Oscar Rwechungura kombe la ushindi wa kwanza taasisi za fedha kwenye kilele cha maonesho ya Kilimo Kanda ya Kaskazini Nanenane Themi mkoa wa Arusha.

4%2B%25287%2529
Sehemu ya madhimiso  ya kilele cha Siku ya Wakulima nchini (Nane nane).
Na Mwandishi Wetu, SIMIYU

BENKI ya NMB imetoa mafunzo kwa zaidi ya Vyama Vya Msingi 1, 000 vya Ushirika wa Wakulima (AMCOS) ya kilimo na utunzaji fedha ndani ya Mwaka mmoja yenye lengo la kuboresha sekta ya kilimo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika madhimiso ya kilele cha siku ya wakulima nchini (Nane nane) Mkoani Simiyu, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB - Ineke Bussemaker alisema benki yake imemaua kusaidia kuboresha sekta ya kilio kutokana na umuhimu wake katika kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi na pia kuboresha uchumi wa wakulima.

Alisema kuwa mafunzo hayo ambayo bado yanaendelea sehemu mbali mbali nchini yanatariwa kuwafikia wakulima wengi zaidi kupitia vyama vya ushirika na hivyo vitawezesha kuboresha kilimo na kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika ngazi ya jamii na nchi kwa ujumla.

Alisema kuwa sekta ya kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa nchi na kuajiri watanzania zaidi ya asilimia 70, hivyo inapaswa kuboreshwa ili kutoa mchangomkubwa katika maendeleo ya kiuchumi.

Bi. Bussemaker alisisitiza kuwa unatakiwa ushirikiano wa wadau mbalimbali wa maendeleo ili kusaidia sekta ya kilimo kukua kwa haraka na kuleta tija kwa wakulima na nchi kwa ujumla na kuwa ikiachiwa serikali peke yake haitaweza kuleta mabadiriko hayo kwa haraka. Alisema kuwa benki yake inaamini kuwa sekta ya kilimo inao uwezo mkubwa wa kuleta mapinduzi ya kweli katika uchumi endapo kilimo kitaboreshwa nchini na kwamba sekta hiyo itakuwa na mchango mkubwa katika kufikia malengo ya serikali ya uchumi wa viwanda.

Bi. Bussemaker alisema kuwa mbali na mafunzo hayo benki yake imekwisha tumia zaidi ya shilingi bilioni 100 katika kuboresha sekta ya kilimo nchini kwa kutoa mikopo mbalimbali pamoja na huduma zingine za kifedha kwa wakulima nchini.

“Ndani ya miaka michache ijayo, tunatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 500 katika sekta kuwezesha shughuli za kilimo katika mnyororo mzima wa thamani, hivyo nawaomba wakulima kuto kukata tamaa na kilimo kwani benki yao ipo pamoja nao katika kuhakikisha inaleta mageuzi ya kilimo kwa manufaa na amendeleo ya wakulima na nchi kwa ujumla” alisema Bi. Bussemaker.

Bi. Bussemaker aliwataka wakulima kutumia NMB Bank katika kuleta mageuzi chanya katika kilimo na kuinua uchumi wa Tanzania kufikia uchumi wa kati kwa kuzalisha malighafi zaidi ndani ya nchi ambazo zitatumika katika viwanda vilivyopo nchini kwa kuwa mkulima akilima zaidi viwanda vinapata malighafi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)